KIJANA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUBAKA WANAFUNZI WA DARASA LA TATU MSITUNI


Kaimu kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Kagera ACP Maketi Msangi


Na Mbuke Shilagi - Kagera.

Jeshi la Polisi Mkoani Kagera linamshikilia mtu mmoja aliye julikana kwa jina la Maiko Martin  (30) mkazi wa mtaa wa Kyabitembe Kata ya Nshambya tarafa ya Rwamishenye Manispaa ya Bukoba kwa tuhuma za kubaka watoto watatu, wanafunzi wa darasa la tatu na nne wenye umri wa kati ya miaka 10 mpaka 12.


Hayo yamethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera ACP Maketi Msangi wakati akizungumza na vyombo vya habari amesema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda tukio hilo mnamo tarehe 23 Februari 2022, katika msitu wa Rwendimi uliopo katika Kijiji cha Ijuganyondo Kata ya Ijuganyondo Manispaa ya Bukoba.


Amesema kuwa watoto hao walienda kuokota kuni katika msitu huo na ndipo mtuhumiwa aliwavizia na kuwakamata watoto hao kisha kuwatishia kuwakata na panga endapo watapiga kelele na kisha kuwabaka na kwamba mara baada ya kutenda tukio hilo mtuhumiwa alikimbia kusikojulikana kwa kuhofia kukamatwa.


ACP Msangi ameongeza kuwa watoto hao walimtambua kwa sura mtuhumiwa huyo na kwamba jeshi la polisi liliendelea na juhudi za kumsaka na mnamo tarehe 24 Mei 2022, mtuhumiwa alikamatwa katika Kijiji cha Kyansozi Kata ya Maruku tarafa ya Kyamtwara Halimashauri ya Wilaya ya Bukoba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments