THPS, SERIKALI WAKUTANA NA WADAU KUPANGA MIKAKATI YA KUPAMBANA NA UVIKO – 19 SHINYANGA….IMANI POTOFU BADO TATIZO, HAMASA YAHITAJIKA ZAIDI


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la THPS, Dkt. Redempta Mbatia akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Mei 27,2022 Mjini Kahama.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kupitia mradi wake wa CDC/ PEPFAR Afya HATUA kwa kushirikiana na kamati za afya za Mkoa na Wilaya za Shinyanga kwa ufadhili wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa UKIMWI (PEPFAR) kupitia Shirika la CDC wameendesha mkutano wa wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga ili kutathmini maendeleo ya utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 na kupanga mikakati mahususi ya kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo hiyo katika mkoa wa Shinyanga.


Mkutano huo ambao umefanyika leo Ijumaa Mei 27,2022 Mjini Kahama na umefunguliwa na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Emmanuel Johnson kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Edward Mjema ambapo kupitia mkutano huo wadau wa afya wamefanya tathmini na majadiliano ya hali ya utolewaji wa chanjo ya UVIKO-19 na kupanga mikakati ya kupambana na ugonjwa wa COVID -19.


Akifungua mkutano huo, Johnson ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kutumia vizuri fursa ya kupatiwa chanjo ya UVIKO-19 maana kwa kufanya hivyo wataweza kuokoa maisha yao.


Amesema Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau unaendelea kutoa chanjo ya UVIKO -19 katika halmashauri zake zote sita na kwamba kwa kushirikiana na Shirika la THPS wameendelea kutoa huduma za VVU na UKIMWI.

“Tuendelee kuhamasisha jamii kuchukua tahadhari juu ya UVIKO – 19. Serikali itaendelea kutoa taarifa kuhusu namna ya kukabiliana na ugonjwa huu kadri inavyowezekana kwa kutumia vyombo vya habari na wataalamu wa afya”,amesema Johnson.

“Jamii nzima inalo jukumu la la kuhakikisha kwamba kila mmoja,kila kaya, kila taasisi wanatekeleza na kufuata taratibu zote za kujikinga na ugonjwa huu bila kulazimisha wala kutumia nguvu za ziada lakini itakaposhindikana tutafanya hivyo kwa mujibu wa sheria ya afya ya jamii ya mwaka 2009 inayozuia mtu kuambukiza ugonjwa mtu mwingine kwa maksudi ambapo anafahamu kuna njia za kujikinga”,amesema Johnson.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Mzee amelishukuru Shirika la THPS kwa ushirikiano wanaoendelea kutoa mkoani Shinyanga hasa katika Huduma za VVU na UKIMWI na mapambano dhidi ya UVIKO – 19 .

Aidha amesema Serikali ya Mkoa wa Shinyanga imejipanga kikamilifu katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID -19 na kwamba kinachotakiwa ni hamasa katika jamii wananchi wajitokeze kupata chanjo.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la THPS, Dkt. Redempta Mbatia ameomba washiriki wa mkutano huo kubuni mipango mahususi itakayowashirikisha viongozi wa jamii na kisiasa katika uhamasishaji wa chanjo ya UVIKO- 19 na kupelekea kupata matokeo chanya katika utolewaji wa chanjo ya UVIKO 19 huku akipongeza nchi ya Tanzania kwa jitihada za utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 ambazo zimepokelewa vyema na kupelekea kuungwa mkono na  wadau wengi.

“Tumekutana hapa kwa ajili ya kupanga mikakati ya namna gani tutaweza kudhibiti kwa pamoja kuhakikisha jamii ya Watanzania hapa mkoani Shinyanga inakingwa na ugonjwa wa UVIKO – 19 kwa kuhakikisha kila mtu anafikiwa na chanjo ya UVIKO – 19. Tunashukuru sana kwa ushirikiano na jitihada zinazofanyika kwenye halmashauri zote na tunaishukuru serikali kwa kuhakikisha jamii inafikiwa na chanjo na kuweka msisitizo mkubwa katika kuwalinda Watanzania”,amesema Dkt. Redempta.

“Kadhalika tunawashukuru wafadhili wetu ambao wamehakikisha chanjo zinafika kwenye nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kwa upande wetu sisi tunaishukuru Serikali ya Marekani, siyo tu kwa kuhakikisha tunapata chanjo lakini pia kuleta rasilimali ambazo zinatusaidia sasa hizo chanjo zimfikie kila mtu kule alipo hata kama ni nyumbani kwake",amesema.

Ameongeza kuwa THPS kwa kushirikiana na mkoa na halmashauri zote mkoani Shinyanga wameyafikia makundi maalumu yaliyokuwa yamelengwa hapo awali, ambapo wamefikia asilimia 79 ya Watu Wanaoishi na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI , asilimia 92 ya watumishi wa Sekta ya Afya (watumishi 1552 mkoani Shinyanga) na kufikia wazee zaidi ya miaka 60 wapatao 9012.

“Pamoja na mafanikio haya safari bado ni ndefu.Mpaka kufikia sasa mkoa wa Shinyanga una idadi ya watu 1,011,085 wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea ambao wanafaa kupata chanjo ya UVIKO-19. Mkoa huu umeweza kuchanja watu 127,071 tu na hii imepelekea kufanya kikao hiki. Changamoto kubwa mkoani Shinyanga tunayokabiliana nayo ni imani potofu kuhusu chanjo hali inayokwamisha wananchi kujitokeza kupata chanjo”,amesema Dkt. Redempta.

“Kati ya malengo ya Mkutano huu ni kutambulisha rasilimali za ziada tulizozipata kupitia Mpango wa Dunia wa Global Vax, kwa upande wa Shinyanga takwimu rasmi zitakuja lakini ni kiasi cha kama Shilingi Bilioni Moja, sasa hii pesa imekuja na malengo ya ziada ya watu takribani 500,000 , hivyo tuna kazi kubwa mbele yetu, na ni jukumu letu sote wakiwemo viongozi wa siasa kuhamasisha wananchi kupata chanjo ambapo sasa wananchi wanafuatwa hadi nyumbani”, ameongeza Dkt. Redempta.


Kiongozi wa Miradi ya Tiba kutoka CDC -Tanzania Dkt. Eva Matiko ameeleza kuwa PEPFAR na CDC wataendelea kusaidia upatikanaji wa huduma ya chanjo ya UVIKO-19 katika vituo vya kutolea huduma za afya na jamii kwa ujumla na kwamba ili kuweza kutumia rasilimali za chanjo ya UVIKO-19, uhusiano madhubuti kati ya serikali za mitaa na mradi wa Afya Hatua unahitajika sana.

Amesema CDC- Tanzania kupitia wadau wake kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanikiwa kujumuisha huduma za chanjo ya UVIKO-19 katika utekelezaji wa programu zake.

“Tangu Septemba 2021, kwa kufuata malengo ya PEPFAR, kipaumbele cha kwanza kilikuwa ni kuongeza utoaji wa chanjo kwa watu wanaoishi na VVU, na watoa huduma za afya ngazi ya jamii ambao hutoa huduma kwa WAVIU. CDC- Tanzania kupitia washirika wake, watasaidia serikali ya Tanzania katika kufikia malengo yake ya utoaji wa chanjo ya UVIKO-19, mkoa wa Shinyanga ukiwa miongoni mwao”,amesema Dkt. Eva.


KUHUSU THPS

THPS ni taasisi ya Kitanzania iliyoanzishwa mwaka 2011 kwa kufuata sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002. THPS inatekeleza kazi zake kwa kushirikiana na Wizara ya afya, Wizara ya  maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto pamoja na Ofisi ya Rais- tawala za mikoa na serikali za mitaa (OR- TAMISEMI), Wizara ya mambo ya ndani-hususan Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza, na Wizara ya afya huko Zanzibar. Dira ya THPS ni kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa Tanzania, kupitia uimarishaji wa mifumo ya sekta ya afya ili kutoa huduma bora za afya zikiwemo zile za VVU/UKIMWI, kifua kikuu, kuzuia ukatili wa kijinsia, afya ya uzazi, mama na mtoto na afya ya vijana. THPS pia inatoa huduma za kuimarisha mifumo ya maabara na usimamizi wa taarifa za afya kwa TEHAMA.


Mradi wa CDC/ PEPFAR Afya HATUA (Oktoba 2021-Septemba 2026) unalenga kutoa huduma bora za afya jumuishi katika vituo vya kutolea  huduma za afya (Kigoma, Pwani na Shinyanga) na huduma ngazi ya jamii(Pwani na Kigoma) Huduma za Kinga, tiba na matunzo za VVU ikiwemo huduma huria za kitatibu za tohara kwa wanaume( Kigoma na Shinyanga) na programu ya DREAMS( Determined, REsilient, Empowere, AIDS-free, Mentored and Safe) mkoani Shinyanga. Programu ya DREAMS inatoa huduma jumuishi na mikakati inayoangalia vichocheo hatarishi vya VVU kwa mabinti wadogo.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Emmanuel Johnson akifungua mkutano wa wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Edward Mjema leo Ijumaa Mei 27,2022 Mjini Kahama. Mkutano huo wenye lengo  la kufanya tathmini na majadiliano ya hali ya utolewaji wa chanjo ya UVIKO-19 na kupanga mikakati ya kupambana na ugonjwa wa COVID -19 umeandaliwa na Shirika la THPS kupitia mradi wake wa CDC/ PEPFAR Afya HATUA kwa ufadhili wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa UKIMWI (PEPFAR) kupitia Shirika la CDC. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Emmanuel Johnson akifungua mkutano wa wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Edward Mjema leo Ijumaa Mei 27,2022 Mjini Kahama kwa ajili ya kufanya tathmini na majadiliano ya hali ya utolewaji wa chanjo ya UVIKO-19 na kupanga mikakati ya kupambana na ugonjwa wa COVID -19
Mkurugenzi wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Emmanuel Johnson akifungua mkutano wa wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Edward Mjema leo Ijumaa Mei 27,2022 Mjini Kahama kwa ajili ya kufanya tathmini na majadiliano ya hali ya utolewaji wa chanjo ya UVIKO-19 na kupanga mikakati ya kupambana na ugonjwa wa COVID -19
Wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini kwenye Mkutano wa kujadili tathmini na majadiliano ya hali ya utolewaji wa chanjo ya UVIKO-19 na kupanga mikakati ya kupambana na ugonjwa wa COVID -19 ulioandaliwa na Shirika la THPS kupitia mradi wake wa CDC/ PEPFAR Afya HATUA kwa ufadhili wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa UKIMWI (PEPFAR) kupitia Shirika la CDC.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania Health Promotion Support(THPS), Dkt. Redempta Mbatia akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Mei 27,2022 Mjini Kahama. Mkutano huo wenye lengo  la kufanya tathmini na majadiliano ya hali ya utolewaji wa chanjo ya UVIKO-19 na kupanga mikakati ya kupambana na ugonjwa wa COVID -19 umeandaliwa na Shirika la THPS kupitia mradi wake wa CDC/ PEPFAR Afya HATUA kwa ufadhili wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa UKIMWI (PEPFAR) kupitia Shirika la CDC 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania Health Promotion Support(THPS), Dkt. Redempta Mbatia akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Mei 27,2022 Mjini Kahama kwa lengo  la kufanya tathmini na majadiliano ya hali ya utolewaji wa chanjo ya UVIKO-19 na kupanga mikakati ya kupambana na ugonjwa wa COVID -19.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania Health Promotion Support(THPS), Dkt. Redempta Mbatia akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Mei 27,2022 Mjini Kahama kwa lengo  la kufanya tathmini na majadiliano ya hali ya utolewaji wa chanjo ya UVIKO-19 na kupanga mikakati ya kupambana na ugonjwa wa COVID -19.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Mzee akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Mei 27,2022 Mjini Kahama kwa lengo  la kufanya tathmini na majadiliano ya hali ya utolewaji wa chanjo ya UVIKO-19 na kupanga mikakati ya kupambana na ugonjwa wa COVID -19. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania Health Promotion Support(THPS), Dkt. Redempta Mbatia, kulia ni Mkurugenzi wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Emmanuel Johnson
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Mzee akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Mei 27,2022 Mjini Kahama kwa lengo  la kufanya tathmini na majadiliano ya hali ya utolewaji wa chanjo ya UVIKO-19 na kupanga mikakati ya kupambana na ugonjwa wa COVID -19. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la THPS, Dkt. Redempta Mbatia, Wa kwanza kulia ni Meneja Miradi Shirika la THPS Mkoa wa Shinyanga Dkt. Amos Scot akifuatiwa na Kiongozi wa Miradi ya Tiba kutoka CDC -Tanzania Dkt. Eva Matiko  na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Emmanuel Johnson
Meneja Miradi Shirika la THPS Mkoa wa Shinyanga Dkt. Amos Scot (kulia),  Kiongozi wa Miradi ya Tiba kutoka CDC -Tanzania Dkt. Eva Matiko (katikati) na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Emmanuel Johnson wakiwa kwenye mkutano wa wadau wa afya mkoa wa Shinyanga.
Kiongozi wa Miradi ya Tiba kutoka CDC -Tanzania Dkt. Eva Matiko
akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Mei 27,2022 Mjini Kahama kwa lengo  la kufanya tathmini na majadiliano ya hali ya utolewaji wa chanjo ya UVIKO-19 na kupanga mikakati ya kupambana na ugonjwa wa COVID -19.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Emmanuel Johnson akiongoza mkutano wa wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Edward Mjema leo Ijumaa Mei 27,2022 Mjini Kahama. 
Meneja Miradi Shirika la THPS Mkoa wa Shinyanga Dkt. Amos Scot
Mkurugenzi Tiba na Matunzo Mradi wa Afya HATUA kutoka Shirika la THPS, Dkt. Frederick Ndossi akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa afya mkoa wa Shinyanga
Msimamizi wa Masuala ya Chanjo Shirika la THPS, Dkt. Hans Maro akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa afya mkoa wa Shinyanga
Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Shinyanga, Timothy Sosoma akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa afya mkoa wa Shinyanga
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa afya mkoa wa Shinyanga
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu, Linno Pius Mwageni akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa afya mkoa wa Shinyanga
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga, Nice Munissy akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa afya mkoa wa Shinyanga
Wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini kwenye Mkutano wa kujadili tathmini na majadiliano ya hali ya utolewaji wa chanjo ya UVIKO-19 na kupanga mikakati ya kupambana na ugonjwa wa COVID -19 ulioandaliwa na Shirika la THPS kupitia mradi wake wa CDC/ PEPFAR Afya HATUA kwa ufadhili wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa UKIMWI (PEPFAR) kupitia Shirika la CDC 
Wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini

Wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini kwenye Mkutano wa kujadili tathmini na majadiliano ya hali ya utolewaji wa chanjo ya UVIKO-19 na kupanga mikakati ya kupambana na ugonjwa wa COVID -19 ulioandaliwa na Shirika la THPS kupitia mradi wake wa CDC/ PEPFAR Afya HATUA kwa ufadhili wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa UKIMWI (PEPFAR) kupitia Shirika la CDC 
Wadau wa afya wa mkoa wa Shinyanga wakipiga picha ya pamoja.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post