JAMES MBATIA ASIMAMISHWA KUJIHUSISHA NA SIASA ZA NCCR - MAGEUZI


Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imebariki uamuzi wa Halmashauri Kuu ya NCCR - Mageuzi ya kumsimamisha Mwenyekiti wa Chama hicho pamoja na Sekretarieti yake yote.

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza amesema ofisi hiyo ya msajili inamsimamisha mwanasiasa huyo kujihusisha na siasa za chama hicho hadi pale uamuzi mwingine ndani ya Chama hicho utakapotolewa.

Ameeleza kuwa uamuzi wa Halmashauri kuu ya chama hicho ulikuwa halali kwa kuwa akidi ya kikao husika ilikuwa imetimia.

Mwishoni mwa wiki iliyopita siku ya Jumamosi Mei 21 mwaka huu, Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi ilimsimamisha Mbatia na makamu Mwenyekiti Bara, Angelina Mtahiwa kutojihusisha na shughuli zozote za chama hadi mkutano mkuu utakapoitishwa ili wajieleze kuhusiana na tuhuma zinazowakabili.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post