MWANAMKE AJERUHIWA KWA RISASI POLISI WAKITAWANYA WANANCHI WAKIPIGA MWIZI WA SIMU SINZA


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro.
 ***
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amethibitisha tukio la Mwanamke aitwaye Mariam mkazi wa Sinza Lion Dar es Salaam kujeruhiwa kwa risasi majira ya saa 12:00 asubuhi ya leo Mei 20, 2022 maeneo ya Sinza Lion, na kusema imempata kwa bahati mbaya baada ya Askari kufyatua risasi juu kwa lengo la kuwatawanya wananchi waliokuwa wanampiga mwizi wa simu.

Kauli hiyo ameitoa hii leo wakati akizungumza, ili kutoa ufafanuzi wa madai yaliyotolewa na mashuhuda wa tukio hilo kwa kusema kwamba mwanamke huyo aitwaye Mariam amejeruhiwa na polisi.


“Ni kweli tukio hilo limetokea na jeshi linaendelea kulifuatilia, lakini ni kwamba askari walifyatua risasi juu katika juhudi za kumuokoa mtuhumiwa na kwa bahati mbaya kuna mwanamke amejeruhiwa ingawa anaendelea vizuri,” amesema Kamanda Muliro.


Aidha Kamanda Muliro akimzungumzia mwizi huyo amesema, “Huyo mtuhumiwa hatujamtambua kwa sababu hajaweza kuongea, alikuwa tayari amepigwa, hawezi kuongea, hivyo tunalichunguza tukio hilo”.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post