WAWILI WAKAMATWA TUHUMA ZA KULAWITI BINTI WA DARASA LA SITA....MWENYEWE ASEMA MAMA YAKE KARUHUSU AFANYE MAPENZI NA BABA MWENYE NYUMBA TU

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi George Kyando
***
Wanaume wawili mmoja mwenye umri wa Miaka 42 na mwingine umri wa Miaka 36 wakazi wa Manispaa ya Shinyanga
wanashikiliwa na jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga kwa tuhuma za kulawiti mtoto wa darasa la sita mwenye umri wa Miaka 14.

Tukio hilo limetokea kwenye kata ya Masekelo Mkoani Shinyanga ambapo Mwenyekiti wa Mtaa wa Luhende Msafiri Nadula amesema alifika na kuzungumza na mtoto huyo ambaye aliwataja watu hao na tayari wameshikiliwa na jeshi la Polisi.

Nadula amesema watuhumiwa hao mmoja ni Baba mwenye nyumba pale familia ya mtoto huyo wamepanga na kwamba wameshirikiana na Polisi wa kata ya Masekelo kuwapata watuhumiwa hao.

"Nilipewa taarifa za mtoto huyo kuwa anarudi nyumbani saa saba usiku tarehe 03.05,2022 nilifika nyumbani nikazungumza na mtoto huyo nikamuonya akasema nimekuelewa mwenyekiti sitorudia tena lakini siku iliyofuata nikapigiwa simu saa tano kuwa mtoto huyo ametoka tena",ameeleza Mwenyekiti.

“Basi asubuhi nikaenda tena nyumbani kwao nikamkuta bado amelala ikabidi nimchukue huyo mtoto ili nijue ni changamoto gani anazokutana nazo hadi kuingia nyumbani saa saba usiku akaniambia mama anashinda kwenye vilabu vya pombe nikamuuliza wewe huwa unaenda wapi usiku akasema kwamba tunaenda kutembea kwa mwarabu siku ya sikukuu alitupa Shilingi Mia saba (700)”,ameongeza.

“Nikaendelea kumhoji akawa anabishabisha lakini baadae akasema sawa mimi nilifundishwa na dada yangu huyo mwarabu ni hawara wangu... basi nikampeleka kwa mtendaji tukaendelea kumhoji akakubali yote hayo kwamba huyo mwarabu ni hawara yake ameshafanya naye mapenzi zaidi ya mara tatu, akasema na baba mwenye nyumba huwa anatoka naye kimapenzi, alinikuta usiku nimelala akanilazimisha kufanya mapenzi lakini mama anajua aliniambia niendelee kufanya mapenzi na baba mwenye nyumba ili nikikua anioe”,ameongeza.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema jeshi hilo limewakamata watuhumiwa huku likiendelea na uchunguzi zaidi ili hatua za kisheria zichukuliwa.

“Ni kweli tukio hilo limetokea kwamba mtoto wa Miaka 14 ni binti mwanafunzi wam darasa la sita (6) alikuwa akilawitiwa na watu wawili mmoja mwenye umri wa Miaka 42 na mwingine ana umri wa Miaka 36 inaonekana tendo hilo nila muda mrefu lilikuwa halijagundulika lakini mpaka sasa tayari watuhumiwa hao wawili wote tumeshawakamata na uchunguzi unaendelea na upelelezi ukishakamilika hatua za kuwafikisha mahakamani zitafanyika” amesema kamanda Kyando.

Chanzo - Misalaba blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post