WATOTO 26,954 KUPEWA CHANJO YAPOLIO KATIKA MANISPAA YA BUKOBA

 

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani


Na Mbuke Shilagi Kagera.

Watoto 26,954 wanatarajiwa kupata chanjo ya matone ya Polio katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba Mh. Hamid Njovu Katika kikao Cha Baraza la Madiwani kilicho fanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Bukoba Mei 18, 2022, amesema kuwa tayari chanjo ya polio imeanza Mei 18 katika Manispaa ya Bukoba na kwamba wanatarajia kufikia watoto 26,954 katika Manispaa ya Bukoba.

Amewataka wazazi wote wenye watoto wenye umri wa miaka mitano kushuka chini wanatakiwa kuhakikisha watoto hao wamepata chanjo hiyo ili iweze kuwakinga na mlipuko wa ugonjwa wa Polio ulio bainika katika nchi jirani ya Malawi.

Naye Mganga Mkuu wa Manispaa ya Bukoba Dkt. Mustafa Waziri amesema kuwa Chanjo ya matone ya Polio itadumu kwa siku nne kuanzia ltarehe 18 mpaka tarehe 21 mwaka huu na kwamba watoto watakaopata chanjo hiyo watawekewa alama pamoja na nyumba ili kuhakikisha watoto wote wamepata chanjo.

Ameongeza kuwa zoezi la Chanjo ya Polio ni ya matone na sio sindano na kwamba sehemu watakayokuwa wakitoa huduma hiyo ya Chanjo ni shule za watoto wadogo, nyumba kwa nyumba, Vituo vya kutoa huduma za Afya pamoja na kwenye mikusanyiko ya watu ikiwemo stendi.  

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments