CRDB YAPUNGUZA MKOPO CHECHEFU,YAPATA FAIDA YA SH. BILION 268 KWA MWAKA HUU



**************

Na Agness Nyamaru, Arusha.

Katika kuelekea mkutano mkuu 27 wa wanahisa taasisi ya fedha ya CRDB imefanikiwa kupunguza asilimia sita ya mikopo chechefu kutoka kwa wateja wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha katika kuelekea mkutano huo mkuu wa wanahisa wa taasisi hiyo, Mkurugenzi mkuu mtendaji wa CRDB,Abdulmajid Nseleka amesema kuwa wamefanikiwa kupunguza mikopo chechefu kutoka asilimia 9 hadi 3 kwa mwaka 2019 hadi 2022.

"Nakupitia hilo tumefanikiwa kupunguza riba kwa kuangalia sekta muhimu inayoleta tija kubwa kwenye uchumi wa nchi ambayo ni kilimo,"alisema Mkurugenzi huyo.

Mkurugenzi Nseleka alisema lengo ni kugusa watu wengi walio kwenye sekta nzima ya kilimo ambapo wakulima wengi watafaidika na huduma wanazotoa wao kama benki ya CRDB.

Alisema wakulima hao watanufaika kwa kununuliwa pembejeo au vitendea kazi mbalimbali na sekta ya pili kunufaika ni pamoja na wafanyakazi ambao wamepunguziwa riba kutoka asilimia 18 hadi 13 huku wanawake wajasiriamali wapunguziwa kutoka asilimia 20 hadi 12.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi CRDB,Ally Laay alisema wamekuwa wakitoa elimu kwa wateja wao ikiwemo wanahisa ambao wapo zaidi ya laki sita.

"Tukitoa elimu kwa wateja itasaidia kuelewa umuhimu wa kuwekeza na namna ya kutumia fursa zinazojitokeza katika benki ya CRDB lengo ni kumfikia mwananchi mzawa nakutumia fursa zilizopo,"

"CRDB tumekuwa tukitoa elimu ya fedha na kufanya semina mahususi ya uwekezaji na wengi wamejifunza juu ya uwekezaji ikiwa yapo maeneo mengi ya kuwekeza ila eneo la hisa limeonekana kuwa na changamoto bado hivyo tunaendelea kutoa elimu juu ya hisa za CRDB," alisema mkurugenzi huyo.

Alisema mbali na kufanikiwa kwa kupata faida kubwa ya sh. Bilion 165 kwa mwaka 2021 na sh.Bilion 268 kwa mwaka huu Laat alitaja Uviko -19 kama changamoto ya kidunia kwani ulichangia kupunguza kasi ya kihuduma.

Tully Mwampamba ni mkurugenzi wa mawasiliano katika taasisi hiyo ya kifedha aliwataka wanahisa kutumia haki yao ya msingi ya kupiga kura katika mtandao wao kuwachagua wajumbe wa bodi ya wanahisa kuanzia mei 18,2022.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments