AZAM FC VS SIMBA SC NGOMA NGUMU, ZATOKA SARE 1-1 CHAMAZI


Na Alex Sonna

MABINGWA Watetezi Simba wameshindwa kutamba ugenini dhidi ya Azam FC baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa uwanja wa Chamazi Complex nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Azam FC walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Simba katika dakika ya 17 bao likifungwa na Mshambuliajia Rodgers Kola,Mshambuliaji wa zamani wa Azam ,John Bocco aliisawazishia timu yake dakika ya 44.

Kipindi cha pili timu zote ziliafanya mabadiliko na kuanza kushambualiana kwa zamu hadi dakika 90 zinamalizika timu hizo zimeweze kugawa pointi moja moja.

Kwa Matokeo hayo Simba wamefikisha Pointi 50 wakizidiwa Pointi 10 na Vinara wa Ligi hiyo Yanga wenye Pointi 60 ,Timu zote zikiwa zimecheza mechi 24 na kubakiwa na mechi sita huku Azam FC wakibaki nafasi ya tano wakiwa na Pointi 33.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments