MPC, INTERNEWS WAFANYA MKUTANO KUADHIMISHA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI


Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (Mwanza Press Club - MPC) kwa kushirikiana na Taasisi ya kihabari ya Internews imefanya Mkutano wa Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari duniani kimkoa Katika Hotel ya Gold Crest Jijini Mwanza.


Mkutano huo ulihudhuriwa na Taasisi mbalimbali za kihabari ikiwemo Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari (UTPC), Taasisi ya Ojadact na Viongozi wa kiserikali.


Katika Mkutano huo mgeni Rasmi alikua ni Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Salumu Kali


Akizungumza katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza (MPC ) Edwin Soko katika Kongamano hilo amewasihi Waandishi wa habari kufanya tafakuri ya kina juu ya kutumia kalamu zao katika kufanya kazi kwa maadili na kuandika habari kwa weledi kutokana na kukua kwa teknolojia.


Ameeleza kuwa Mitandao ya kijamii isiwafanye kusahau maadili ya uandishi badala yake wahabarishe, waelimishe na waburudishe Umma kama inavyowapasa kufanya kama Waandishi.


Kwa upande wake Mratibu wa taasisi ya kihabari ya Internews Shaaban Maganga amesema, katika kipindi hiki ambacho dunia inaungana kwa ajili ya kuadhimisha uhuru wa habari wanafurahi, kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza (MPC) katika kuwajengea uwezo waandishi wa habari kwa kuboresha utendaji kazi wa waandishi wa habari.


Amesema dunia ipo katika mabadiliko ya sayansi na teknolojia hivyo matumizi ya mawasiliano kwa njia mtandao ni mhimu kwa sasa katika kuhabarisha tasnia ya habari


Akifungua Mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Magu Salum Kalli amewaasa Waandishi wa Habari kuandika habari zenye ukweli ambazo zinafuata misingi yote ya uandishi wa habari Ili kuepuka migongano katika jamii.


DC Kalli amewataka Waandishi wa habari Mkoani hapa kuwa na naamna Bora ya upashaji habari kwani nafasi yao ni kubwa katika kujenga Mkoa na Taifa Zima kwa ujumla.


"Mhakikishe mnachuja habari zenu kabla hazijarushwa kwenye mitandao ya kijamii au vyombo vya habari maana upo uwezekano mkubwa wa kujenga au kubomoa amani " amesema DC Kalli.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments