Wananchi wakitaka kumshushia kichapo Askari wa Jeshi la Zimamoto mara baada ya kufika eneo la tukio akiwa na Bodaboda bila ya kuwa na Gari la kuzimia moto.
Wananchi wakitaka kumshushia kichapo Askari wa Jeshi la Zimamoto mara baada ya kufika eneo la tukio akiwa na Bodaboda bila ya kuwa na Gari la kuzimia moto.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Watu nane wamenusiurika kifo wakati nyumba ambayo wanaishi mtaa wa Mwinamila Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga ikiungua moto na kuteketeza kila kitu ndani.
Amesema moto huo ulianza kushika kwenye sofa, ndipo ikabidi akimbie kwenda kuzima umeme (Main Switch), na kuanza kuomba msaada kwa wasamaria wema kusaidia kuuzima moto huo, na kufanikiwa kuuzima huku ukiwa tayari umeshateketeza kila kitu ndani, lakini nyumba yao ikisalimika kuteketea.
“Kwenye hii nyumba tunaishi jumla ya watu nane wakiwamo na wapangaji, na huu moto ulianza kuwaka kwenye chumba changu, nashukuru Mungu nyumba haijateketea yote bali zimepotea samani zote za ndani,”anasema Paul.
Naye shuhuda wa tukio hilo la Moto Oscar Kunze, amesema alikuwa amekaa jirani na nyumba hiyo akimsubiri mtu, lakini akasikia kelele nyumba hiyo inaungua moto, ndipo alipofika eneo la tukio na kuanza kusaidia kuuzima, huku watu wengine wakiendelea kwenda na kufanikiwa kuuzima.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo wa Mwanamila eneo ambalo nyumba imeungua moto Lukia Athumani, amewapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi na kuokoa nyumba hiyo isiteketee kwa moto, huku akilitupia lawama Jeshi la Zimamoto na uokoaji kwa kuchelewa kufika eneo la tukio, na moto huo kuzimwa na wananchi.
Amesema amesikitishwa na Jeshi la Zimamoto na uokoaji kwa kutopokea simu kwa wakati, na baada ya kupata taarifa hawakwenda kwa haraka na kuchelewa kufika eneo la tukio, na walipofika walikuwa wamepanda kwenye bodaboda bila ya kuwa na gari, na kusababisha wananchi kutaka kuwashushia kichapo lakini alizuia tukio hilo.
Naye Afisa wa Zimamoto ambaye alinusurika kichapo kutoka kwa wananchi ambaye hakutaka kutaja jina lake, amesema Jeshi hilo linakabiliwa na uhaba wa magari ya kuzimia moto.
Ametolea pia ufafanuzi sakata la Askari wa Jeshi hilo kutaka kupigwa na wananchi wakati alipofika eneo la tukio bila kuwa na gari la kuzimia moto, amesema kuwa Askari huyo alikuwa na wenzake wakitoa mafunzo kwa wananchi namna ya kukabiliana na majanga ya moto karibu na eneo la nyumba hiyo iliyoungua moto na walipopata taarifa ilibidi afike hapo haraka ili kutoa msaada wa awali.
Amesema katika matukio ya moto huwa kuna vitu vingi vya kuwahi kutoa msaada, ikiwemo namna ya kuokoa vitu au watu wasidhurike na moto na ndiyo maana Askari huyo aliwahi ili akatoe msaada wakati askari wengine wakifanya mawasiliano ya kupata gari la kuzimia moto kutoka Jeshi la wananchi kambi ya Kizumbi.
Fred Paul akielezea namna moto ulivyoanza kuwaka kwenye nyumba yao.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwinamila Lukia Athumani akielezea tukio hilo la Moto.
Osca Kunze akielezea namna wananchi walivyofanikiwa kuzima moto.
Fred Paulo akiangalia samani za ndani ambazo zimeteketea wakati nyumba yao ikingua moto.
Wananchi wakiwa eneo la tukio.
Wananchi wakiendelea kuuzima Moto.
Wananchi wakiendelea kuuzima Moto.
vitu vikiwa vimeteketea na moto.
vitu vikiwa vimeteketea na moto.
vitu vikiwa vimeteketea na moto.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
Social Plugin