BAKWATA MWANZA YAWAKUTANISHA WANANDOA KONGAMANO LA 'USIKU WA RAHA'... KIVULINI YATAKA WAONGEZE MAHABA NYUMBANI

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa Mwanza limewakutanisha wanandoa kupitia kongamano maalum la 'Usiku wa Raha' lengo likiwa ni kuimarisha mahusiano miongoni mwa wanandoa.

Akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika Mwanza Hotel Mei 04, 2022, Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke alisema BAKWATA inalenga kuresha misingi ya ndoa kama ilivyokuwa zamani ambapo ndoa zilidumu jambo ambalo siku hizi imekuwa ni changamoto kubwa kwani ndoa zimekuwa na migogoro na huvunjika kwa muda mfupi na kusababisha hatari ya watoto kukosa malezi kutoka kwa wazazi.

Ili kudumisha misingi ya ndoa, Sheikh Kabeke aliwahimiza wanandoa kila mmoja kutimiza wajibu wake ambapo alitaja baadhi ya mambo muhimu ambayo mme na mke kila mmoja anapaswa kuyatimiza ili kulinda ndoa yake.


"Kwa mwanaume lazima awe na uwezo wa kumhudumia mke wake kwa kumlisha/ chakula, kumvisha, kumsikiliza mkewe na kukubali kufanya mashauriano naye inapotokea changamoto. Lakini pia mke anapaswa kuzingatia usafi wa mwili, mazingira kama vile chumba cha kulala na choo pamoja na kutumia vyema ulimi wake anapozungumza na mmewe kwa kuwa na matamshi yenye heshima kwa mmewe", alidokeza Sheikh Kabeke.


Hata hivyo Sheikh Kabeke aliwatahadharisha wanaume hususani waislamu ambao imani yao inawaruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja kwamba wanapaswa kuwa na uwezo wa kuwahudumia kwa usawa wake zao kwa chakula, mavazi na tendo la ndoa lakini pia kuwapa makazi kwani hairuhusiwi wote kukaa nyumba moja labda kama wamekubalina wenyewe huku akijiepusha kuwafitinisha.


Akitoa mada ya ndoa kwenye kongamano hilo la Usiku wa Raha kwa wanandoa, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally alisema :
"Wanandoa wengi wakiwa ndani hawataniani kama wanavyofanya wakiwa nje. Unakuta mwanaume anamtania mama ntilie lakini akirudi nyumbani ni mwendo wa kipolisi polisi, hiyo inapunguza mahaba ndani ya ndoa".


"Hivi lini umesema ahsante kwa mkeo ama mmeo kwa kukupa vyema tendo la ndoa? Ama lini umekuwa muwazi kwake na kumwambia leo umenibip? Lazima wanandoa wazungumze na kutaniana ili kuimarisha mahusiano yao huku kila mmoja akitimiza wajibu wake", Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally aliwahoji wanandoa kwenye kwenye kongamano hilo la Usiku wa Raha, na kuzua vicheko ukumbini.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
"Tumefanya kampeni Mkoa wa Mwanza ya kupeleka ujumbe wa malezi bora, tabia njema na misingi ya ndoa tukishirikiana na Shirika la KIVULINI chini ya Mkurugenzi wake Yassin Ally. Tumesaidia kurejesha misingi na maadili kwa wanandoa" alisema Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke.
"Wanandoa wengi wakiwa ndani hawataniani kama wanavyofanya wakiwa nje. Unakuta mwanaume anamtania mama ntilie lakini akirudi nyumbani ni mwendo wa kipolisi polisi, hiyo inapunguza mahaba ndani ya ndoa" alisema Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally wakati akitoa mada ya ndoa kwenye kongamano hilo la Usiku wa Raha kwa wanandoa.
"Hivi lini umesema ahsante kwa mkeo ama mmeo kwa kukupa vyema tendo la ndoa? Ama lini umekuwa muwazi kwake na kumwambia leo umenibip? Lazima wanandoa wazungumze na kutaniana ili kuimarisha mahusiano yao huku kila mmoja akitimiza wajibu wake" Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally aliwahoji wanandoa kwenye kwenye kongamano hilo la Usiku wa Raha, na kuzua vicheko ukumbini.
Wanandoa wakifuatilia kongamano la 'Usiku wa Raha' jijini Mwanza.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments