WAZIRI NAPE AWAKALIA KOONI MAAFISA HABARI...ATOA SIKU 14 MITANDAO YA KIJAMII


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ametoa siku 14 kwa Haafisa Habari nchini kuhakikisha kila tovuti ya serikali na mitandao ya kijamii inakuwa na taarifa zinazoendana na wakati huku akiahidi kuwashughulikia Maafisa Habari watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo.

Pia waziri Nape amewataka maafisa habari wa serikali wasiruhusu watu wapotoshe mafanikio ya serikali na badala yake wametakiwa kujibu hoja ili kuwaelewesha wananchi.

Waziri Nape ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akifungua kikao cha 17 cha maafisa habari, mawasiliano na uhusiano wa serikali kinachoketi kwa siku tano jijini Tanga.

Awali akifungua kikao hicho Waziri Nape amesema kumekuwa na tatizo sugu la muda mrefu katika tovuti na mitandao ya kijamii za wizara na taasisi mbalimbali za serikali kuwa na habari zilizopitwa na wakati.

"Nitoe siku 14 kuanzia tarehe 14.5 kila tovuti ya serikali au taasisi ya serikali au serikali za mitaa iwe na taarifa zinazoendana na wakati afisa habari atakayeshindwa kutekeleza hili ndugu Msigwa hatutaweza kuendelea naye inabidi tuachane naye, "amesema Waziri Nape.

Aliongeza kuwa najisikia vibaya sana ninapopita na kusikia kuna taasisi za serikali tovuti za Mkoa za wizara, Wilaya au Halmashauri zina taarifa za miaka miwili au mitatu iliyopita halafu tuna afisa habari kwenye hilo eneo haiwezekani jamani na tusipoambiana tutakuwa hatutendeani haki jamani sasa siku 14 zinatosha kabisa Msigwa ulikague na nipate taarifa ya jambo hili.

Ameongeza kuwa nasikitika kuona tovuti ya wilaya, Mkoa, Halmashauri haziendani na wakati watu wengi wameacha kutembelea tovuti za serikali kwajili ya kuwepo taarifa zilizopitwa na wakati tutoke kwenye aibu hiyo tumewafanya watu hawatembelei tovuti za serikali halafu tuna afisa tena anajiita afisa habari, "amesisitiza Waziri Nape.

"Mhakikishe mnajibu hoja za wananchi kwenye vyombo vya habari kwa wakati muafaka kuhusu changamoto zinazojitokeza msiruhusu watu wapotoshe ukweli kwani ukweli unapopotoshwa ni aibu kwa maafisa habari supu inanywewa ya moto usisubiri mpaka usukumwe kwenda kukanusha habari ambayo ni ya uongo akikibu saa moja saa mbili nawe sema tukiends hivyo watakuwa na nidhamu kwenye kupotosha, "alisisitiza Waziri Nape.

Aidha Waziri Nape ameagiza utengenezwe utaratibu wa mafunzo kwa maafisa habari nchi nzima juu ya miradi mikubwa ya kitaifa inayotekelezwa na serikali ili wawe na uelewa wa kuisemea miradi hiyo wakati wowote.

"Sote tunafahamu katika mwaka mmoja wa Rais Samia ameleta mageuzi makubwa ambayo tumeyashuhudia jukumu letu ni kuhakikisha Lengo la kufanya hivi ni kwamba tunataka kila afisa habari hata anapoamshwa usingizini awe anaijuanikiamini tukifanya hivyo tutawapa uwezo wa kitu cha kusema, "amebainisha waziri Nape.

CHANZO - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments