Breaking

Post Top Ad

Saturday, May 14, 2022

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MGENI RASMI MAADHIMISHO SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI


Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya siku ya uhuru wa habari duniani kwa upande wa Zanzibar Faroq Qareem akizungumza

**

Na Rahma Idrisa Haji - Zanzibar

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Othman Masoud Othman anatarajiwa kuwa mgeni rasmi siku ya uhuru wa habari duniani kwa upande wa Zanzibar Jumapili Mei 22,2022.


Akitoa taarifa ya madhimisho hayo mbele ya vyombo vya habari katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar ( SUZA )Idara ya mawasiliano na mafunzo ya habari kilichopo kilimani Mkoa wa Mjini Magharibi Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya siku ya uhuru wa habari duniani kwa upande wa Zanzibar Faroq Qareem amesema kuwa  Madhimisho hayo yanategemewa kufanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil kuanzia saa 2:30 Asubuhi Mei 22,2022.

Amesema kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anategemewa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman ambapo waandishi wa habari mbalimbali watahudhuria ikiwemo wadau wa Habari kutoka katika asasi za Kiraia kutoka Zanzibar.

"Maadhimisho haya ya mwaka huu yataambatana  na uwasilishwaji wa mada mbili ambazo ni hali ya uandishi wa kwa Zanzibar ikiwemo matumizi ya Teknolojia na mapungufu ya sheria ya habari, hata hivyo kutakuwa na ushuhuda wa waandishi wa habari katika mafanikio na changamoto zao wakati wa kutekeleza majukumu yao",amesema

Qareem amesema kuwa Maadhimisho ya mwaka huu yamebeba ujumbe muhimu ambao ni UANDISHI WA HABARI NA CHANGAMOTO ZA KIDIGITI Lakini kwa Upande wa Zanzibar kuna kauli mbiu isemayo UANDISHI WA HABARI ZANZIBAR MUELEKEO NA CHANGAMOTO.

Akizungumzia kuhusu shindano la Tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari amesema kuwa mara hii tuzo hizo zitafanyika tarehe 28 mwezi wa 9 mwaka huu ambapo ni kilele cha siku ya kujua duniani (WORLD RIGHT TO KNOW DAY ) kwa lengo la kuwapa fursa waandishi wengi kuweza kushiriki shindano hilo .

"Tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari zitakuwa katika vipengele vifuatavyo

TUZO YA UCHUMI WA BULUU ( DK MWINYI AWARD )

TUZO YA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ( MAALIM SEIF AWARD )

TUZO YA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA ( ZAEKA AWARD )

TUZO YA KULIPA KODI  ( ZRB AWARD )

TUZO YA UKIMWI NA AFYA

TUZO YA UWAJIBIKAJI ( SECOND VICE PRESIDENT AWARD )

TUZO YA MAZINGIRA ( FIRST VICE PRESIDENT AWARD )

TUZO YA JINSIA

TUZO YA UTAWALA BORA NA HAKI ZA BINAADAMU.

 Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages