YANGA SC YAANDAA PUNGUZO LA JEZI KUELEKEA KARIAKOO DERBY**********

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU imewataka mashabiki wa Yanga kuhakikisha wanaingia uwanjani kwa wingi hasa ukizingatia wao ndo wenyeji wa mchezo ujao dhidi ya watani wao wa Jadi Simba Sc, mchezo ambao utapigwa Jumamosi Aprili 30,2022 katika dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo na Waandishi wa habari kuelekea mchezo huo, Msemaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara amesema mashabiki wa Yanga Sc wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye michezo kadhaa kwenye ligi hivyo amewataka kuendelea kujitokeza kushuhudia timu hiyo ikifanya vizuri kwenye ligi ya NBC ambapo Yanga inaongoza kwa tofauti ya pointi 13.

"Tunakusudia kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba SC sisi kama wenyeji tuwe na Mashabiki wengi zaidi uwanjani na kutakuwa na Promotions nyingi kuelekea mchezo huu na Mashabiki wetu watafaidika sana na promotions hizo". Amesema Haji Manara.

Manara amesema mpaka sasa hawajafikisha pointi nyingi ambazo wenzao vilabu 15 wanaweza kuzifikia hiyo ina maana mpaka sasa bado wapo kwenye kuwania Ubingwa.

"Tutakuwa na Punguzo la Bei Maalum ambapo Mshabiki wa Yanga utajipatia Jezi ya msimu huu na Tiketi ya Mzunguko kwa Shillingi 25,000 tu na pia tutakuwa na Punguzo Maalum kwa Jezi za Msimu Uliopita na tiketi ya Mzunguko kwa shilingi 15,000 tu.
Hii ni Special Offer na Zawadi kwa Mashabiki wetu kuelekea mchezo wetu wa Jumamosi dhidi ya Simba SC". Amesema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post