DC MAGU : BAKWATA SISITIZENI ELIMU DUNIA NA DINI

Mkuu wa Wilaya Magu, Salum Kalli amewahimiza waumini wa dini ya kiislamu kutoa nafasi sawa kwa watoto wao kupata elimu ya dini pamoja na elimu dunia ili kutoa fursa kwa Taifa kuwa na wataalamu wa kada mbalimbali.

Kalli alitoa rai hiyo Jumapili Aprili 24, 2022 wakati akizungumza kwenye kongamano la ‘malezi bora, tabia njema na misngi ya ndoa’ lililofanyika katika msikiti mkuu wa BAKWATA wilayani Magu.


Alishauri viongozi wa BAKWATA kuwahimiza waumini waumini wao kutafuta elimu dunia na elimu dini kwani kwa kufanya hiyo itasaidia Taifa kuwa na jamii ya watu walioelimika na wanaozingatia maadili ya pande zote mbili na hivyo kutimiza ipasavyo wajibu wao ikiwemo malezi bora na kujiletea maendeleo.


Aisha Kali aliwahimiza wananchi wakiwemo waumini wa dini ya kiislamu kushiriki ipasavyo kwenye zoezi la Sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu 2022 ambapo alitoa rai kwa viongozi wa dini kuendelea kuelimisha waumini wao kujiandaa na zoezi hilo.


Naye Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke alisema elimu dunia pia ni jambo la msingi kwa jamii ya waislamu akisema “tuna mkakati wa kujenga vituo vya afya kila wilaya mkoani Mwanza, bila kusomesha watoto tutawapa wapi madaktari, manesi na wafamasia”.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally alisema ni vyema BAKWATA ikasisitiza wanafunzi kwenda shule katika siku za wiki (Jumatatu hadi Ijumaa) na siku za wikendi (Jumamosi na Jumapili) wakaenda madrasa hatua itakayosaidia kushindana vyema kielimu na wenzao.


Makongamano ya ‘malezi bora, tabia njema na misingi ya ndoa yanafanyika katika Wilaya zote mkoani Mwanza yakiandaliwa na BAKWATA kwa kushirikiana na KIVULINI kwa lengo la kuelimisha jamii kupinga ukatili wa kijinsia, maelewano ndani ya ndoa, wazazi kulea watoto wao ili kuondoa utoro mashuleni na watoto wa mitaani ambapo maoni yanayokusanywa yatawasilishwa kwa Katibu Tawala Mkoa Mwanza ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya MTAKUWWA kwa ajili ya utekelezaji zaidi.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Magu, Salum Kalli akizungumza kwenye kongamano hilo.
Waumini wa dini ya kiislamu wilayani Magu wakifuatilia kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiwasilisha mada ya malezi kwenye kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiwasilisha mada wakati wa kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akizungumza kwenye kongamano hilo.
Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke akisisitiza jamii kurejesha maadili kama ilivyokuwa zamani hatua itakayosaidia kuondoa mifarakano kwenye ndoa.
Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke (katikati) akizungumza kwenye kongamano hilo.
Waumini wa dini ya kiislamu wilayani Magu wakifuatilia kongamano la 'malezi bora, tabia njema na misingi ya ndoa' lililofanyika katika Msikiti Mkuu wa BAKWATA wilayani humo.
Sheikh wa Wilaya Magu, Nuhu Zaidi alitoa rai kwa jamii kuzingatia mafundisho yaliyowasilishwa kwenye kongamano hilo.
Viongozi mbalimbali wakifuatilia kongamano hilo.
Waumini wa dini ya kiislamu wilayani Magu wakifuatilia kongamano hilo.
Waumini wa dini ya kiislamu wilayani Magu wakifuatilia kongamano la malezi bora lililoandaliwa na BAKWATA Mkoa Mwanza kwa kushirikiana na shirika la KIVULINI katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani ambapo makongamano ya aina hiyo yanafanyika katika Wilaya zote za Mkoa Mwanza.
Waumini wa dini ya kiislamu wilayani Magu wakifuatilia kongamano hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post