MWANAUME APONDWA NA KUCHEMSHWA HADI KUFA ...MABAKI YA VIPANDE VYA MWILI WAKE KUZIKWA LEO


Caleb Otieno, mwanaume aliyepondwa na kuchemshwa hadi kufa katika tanuri ya kampuni ya Blue Nile Rolling Mills mjini Thika atazikwa nyumbani kwao eneo la Kogony katika Kaunti ya Kisumu leo Jumamosi, Aprili 9,2022.

Mabaki ya mwili wake yaliondoka katika hifadhi moja ya maiti mjini Thika mnamo Ijumaa na kusafirishwa hadi nyumbani kwao kwa ajili ya mazishi.

 Otieno alikuwa na kibarua cha kuweka vipande vya chuma katika moto mkali na siku ya kufa kwake mnamo Machi 25,2022 alikuwa kazini kama kawaida.

 Inaarifiwa dakika chache kabla ya kifo chake, alimpa mwenzake KSh 50 sawa na shilingi 1000 ya Tanzania ili amnunulie chakula cha mchana.

Mfanyakazi mwenzake aliporudi na Ugali, mboga, pojo zilizochemshwa na maharagwe, Otieno hakuwepo tena. 

Alipokuwa akiweka vipande vya chuma kupitia kinu cha kuviringisha kwenye tanuri inayowaka, glavu zake zilikwama kwenye vyuma.

 Hapo ndipo vinu vilipomvuta kwenye mashine ambayo ilimponda vipande vipande kabla ya kumwangusha katika tanuri.

 DCIO wa kaunti ndogo ya Thika Joseph Thuvi aliambia gazeti la the Star kuwa walifika eneo la mkasa na kukusanya chembechembe ambazo zilionekana kuwa vipande vya mifupa kutoka kwa tanuri hiyo. 

Kwa mujibu wa chapisho hilo, Thuvi alisema kuwa suala hilo litashughulikiwa tu kama kisa cha ajali za kawaida kazini.

 Inaarifiwa kampuni hiyo imeiambia familia ya mwendazake kwamba itakuwa ikiwalipa shilingi elfu saba kila mwezi kwa miaka mitano kama fidia.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post