MBUNGE WA BARIADI MHANDISI KUNDO AKABIDHI MABATI UJENZI WA ZAHANATI NYANGUGE...AWAPONGEZA WANANCHI KUCHANGIA UJENZI

Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mhandisi Kundo Mathew (mwenye kanzu nyeupe) akikabidhi mabati 150 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nyanguge wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu


Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
MBUNGE wa Jimbo la Bariadi Mhandisi Kundo Mathew amewapongeza wananchi wa kijiji cha Nyanguge katika wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kwa kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji chao ambayo imekamilika katika hatua ya boma.


Mhandisi Kundo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano amesema serikali na wadau wa maendeleo wanatakiwa kuwaunga mkono wananchi hao ili wasipoteze nguzu na fedha walizochangia.


Mhandisi Kundo ameyasema hayo leo (April 29, 2022) mara baada ya kukabidhi mabati zaidi ya 150 kwa ajili ya kukamilisha upauaji wa jengo hilo ambalo limejengwa kwa michango na nguvu za wananchi.


"Niwapongeze sana wananchi wa kijiji hiki mmekuwa mfano wa kuigwa katika jimbo la Bariadi, mmejitolea kuchangia ujenzi wa jengo la zahanati ambalo limefikia hatua ya upauaji, serikali iko pamoja nanyi na pia bado ujenzi na ukamilishaji wa zahanati hii unaendelea, hivyo tutaendelea kuchangia zaidi na zaidi’’, amesema Mhandisi Kundo.


Mhandisi Kundo ametimiza ahadi yake aliyoitoa Januari mosi wakati sherehe mwaka mpya, ambapo wananchi wa kijiji hicho kuzitumia kwa ajili ya kusherehekea, kushiriki na kuchangia miradi ya maendeleo kijijini hapo.


Mwenyekiti wa Kikundi cha Nyanguge Mtandao ambao ni wachangiaji wa maendeleo ya Kijiji hicho, Mlanda Shigukulu alimpongeza Mbunge wa jimbo hilo kwa namna alivyowashika mkono na kutimizai ahadi ya kuchangia mabati kwa ajili ya ukamilishaji wa zahanati hiyo.

Mlanda amesema wananchi, wafanyabiashara na wasomi wa kijiji hicho wameshikamana kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ambapo kila mmoja ameshiriki ujenzi wa zanahati hiyo kwa namna tofauti na kwamba hadi sasa jengo hilo limegharimu zaidi ya milioni 12.
Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mhandisi Kundo Mathew (mwenye kanzu nyeupe) akikabidhi mabati 150 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nyanguge wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu leo.
Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mhandisi Kundo Mathew (mwenye kanzu nyeupe) akikabidhi mabati 150 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nyanguge wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu leo.
Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mhandisi Kundo Mathew akiongea na wananchi wa kijiji cha Nyanguge wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu mara baada ya kukague ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho, kulia ni Diwani wa kata ya Ngulyati Mganga Ndamo.
Jengo la zahanati ya Kijiji cha Nyanguge
Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mhandisi Kundo Mathew akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Nyanguge wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments