Picha : MAFUNZO KWA VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA SHINYANGA YAFUNGWA, WATAKIWA KUZINGATIA KIAPO CHA AHADI YA UADILIFU

Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Mkoa wa Shinyanga, Solomon Lwenge akiwaapisha kiapo cha Ahadi ya Uadilifu Wajumbe wa Bodi za vyama vya Ushirika na wajumbe wa kamati mbalimbali leo Ijumaa Aprili 29,2022 katika ukumbi wa SHIRECU Mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mafunzo ya Uongozi kwa Viongozi wa Vyama vya Ushirika (Wajumbe wa Bodi za vyama vya ushirika na wajumbe wa kamati mbalimbali) mkoa wa Shinyanga yamehitimishwa leo Ijumaa Aprili 29,2022 kwa viongozi hao kula kiapo cha uadilifu ili kutekeleza majukumu yao kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuepuka vitendo vya rushwa,migongano ya kimaslahi na kufuata sheria mbalimbali.


Akizungumza wakati wa kuwaapisha viongozi hao kiapo cha Ahadi ya Uadilifu, Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Mkoa wa Shinyanga, Solomon Lwenge amewataka Wajumbe wa Bodi za vyama vya Ushirika na wajumbe wa kamati mbalimbali kuzingatia kiapo hicho na endapo wataenda kinyume basi watachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwenye nafasi za uongozi.

“Ukienda kinyume na kiapo hiki unatenda kosa la jinai. Hakikisheni mnafanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma. Hakikisheni mnazingatia matakwa ya vifungu vya sheria ya vyama vya ushirika Na. 6 ya mwaka 2013, Kanuni za Vyama vya Ushirika za mwaka 2015 na sheria zingine za nchi katika kutekeleza na kusimamia shughuli za uendeshaji wa vyama vya ushirika”,amesema Lwenge.

Kwa upande wake Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace amewataka viongozi wa Vyama vya Ushirika kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Masharti na Sera za Vyama vya Ushirika sambamba na kulinda rasilimali za vyama na kujiepusha na vitendo vya rushwa na kutanguliza mbele maslahi ya chama kwa kuepuka maslahi binafsi.

Naye Mwakilishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga Bi, Hilda Mfuruki amesema TAKUKURU haitasita kuchukua hatua kwa Viongozi wa vyama vya Ushirika watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa huku akiomba wana ushirika kutoa taarifa TAKUKURU wanapobaini kuna vitendo vya rushwa.


Mafunzo ya siku mbili kwa viongozi wa vyama vya ushirika mkoa wa Shinyanga yalifunguliwa Alhamisi Aprili 28,2022 na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya usimamizi wa Ushirika, kujiendesha kibiashara na Maadili ili waweze kufanya shughuli zao vizuri.

Katika mafunzo hayo Wajumbe wa Bodi za vyama vya ushirika na wajumbe wa kamati mbalimbali mkoa wa Shinyanga wamejengewa uwezo kuhusu maadili ya utumishi,namna ya kujiendesha kibiashara pamoja kukutanishwa na wadau mbalimbali wa Sekta ya Kilimo zikiwemo Taasisi za Kibenki ili kuonesha fursa walizonazo kwa wakulima ili waweze kulima kwa tija na kibiashara zaidi.

Katika mafunzo hayo ,Vyama vikuu vya Ushirika SHIRECU na KACU, Mradi wa pamoja Tanzania(TANCCOPS), Chuo Kikuu cha Ushirika MoCU, Shirika la ukaguzi  COASCO, ASA, TOSCI, AGRICOM, NIC, NHIF, NMB, NBC,CRDB, EQUITY Bank na Shirikisho la vyama vya ushirika Tanzania walishiriki katika kutoa mada muhimu kwa viongozi wa bodi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Mkoa wa Shinyanga, Solomon Lwenge akizungumza wakati akiwaapisha kiapo cha Ahadi ya Uadilifu Wajumbe wa Bodi za vyama vya Ushirika na wajumbe wa kamati mbalimbali leo Ijumaa Aprili 29,2022 katika ukumbi wa SHIRECU Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Mkoa wa Shinyanga, Solomon Lwenge akizungumza wakati akiwaapisha kiapo cha Ahadi ya Uadilifu Wajumbe wa Bodi za vyama vya Ushirika na wajumbe wa kamati mbalimbali leo Ijumaa Aprili 29,2022 katika ukumbi wa SHIRECU Mkoa wa Shinyanga. Kushoto ni Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace.
Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Mkoa wa Shinyanga, Solomon Lwenge akiwaapisha kiapo cha Ahadi ya Uadilifu Wajumbe wa Bodi za vyama vya Ushirika na wajumbe wa kamati mbalimbali leo Ijumaa Aprili 29,2022 katika ukumbi wa SHIRECU Mkoa wa Shinyanga.
Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Mkoa wa Shinyanga, Solomon Lwenge (wa pili kushoto) akiwaapisha kiapo cha Ahadi ya Uadilifu Wajumbe wa Bodi za vyama vya Ushirika na wajumbe wa kamati mbalimbali leo Ijumaa Aprili 29,2022 katika ukumbi wa SHIRECU Mkoa wa Shinyanga.
Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Mkoa wa Shinyanga, Solomon Lwenge (wa pili kushoto) akiwaapisha kiapo cha Ahadi ya Uadilifu Wajumbe wa Bodi za vyama vya Ushirika na wajumbe wa kamati mbalimbali leo Ijumaa Aprili 29, 2022 katika ukumbi wa SHIRECU Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wa Bodi za vyama vya Ushirika na wajumbe wa kamati mbalimbali wakila kiapo cha Ahadi ya Uadilifu 
Wajumbe wa Bodi za vyama vya Ushirika na wajumbe wa kamati mbalimbali wakila kiapo cha Ahadi ya Uadilifu 
Wajumbe wa Bodi za vyama vya Ushirika na wajumbe wa kamati mbalimbali wakila kiapo cha Ahadi ya Uadilifu 
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace akiwasisitiza Viongozi wa Vyama vya Ushirika kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace akizungumza wakati wa mafunzo kwa viongozi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga.
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace akizungumza wakati wa mafunzo kwa viongozi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga.
Viongozi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace akizungumza wakati wa mafunzo kwa viongozi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Singida, Yahaya Ramadhani akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Shinyanga (SHIRECU) Kwiyolecha Nkilijiwa na Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) Hamis Majogoro Mbogola wakitambulishwa wakati wa mafunzo kwa viongozi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) Hamis Majogoro Mbogola akitoa salamu wakati wa mafunzo kwa viongozi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Shinyanga (SHIRECU) Kwiyolecha Nkilijiwa akitoa salamu wakati wa mafunzo kwa viongozi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Singida, Yahaya Ramadhani akitoa salamu wakati wa mafunzo kwa viongozi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga.
Mwakilishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga Bi, Hilda Mfuruki akiwasisitiza viongozi wa vyama vya Ushirika kuepuka vitendo vya Rushwa.
Mmoja wa viongozi wa vyama vya Ushirika akichangia hoja wakati wa mafunzo
Mmoja wa viongozi wa vyama vya Ushirika akichangia hoja wakati wa mafunzo
Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Mkoa wa Shinyanga, Solomon Lwenge akipiga picha ya pamoja na Wadau wa Sekta ya Kilimo (Wadau wa Ushirika).
Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Mkoa wa Shinyanga, Solomon Lwenge akipiga picha ya pamoja na viongozi wa vyama vya Ushirika.
Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Mkoa wa Shinyanga, Solomon Lwenge akipiga picha ya pamoja na viongozi wa vyama vya Ushirika.
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace akipiga picha ya pamoja na viongozi wa vyama vya Ushirika
Picha ya kumbukumbu

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Soma pia:
Picha : VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA SHINYANGA WAPATIWA MAFUNZO, RAS ATAKA WAWE WAAMINIFU, WAAJIRI WATENDAJI WENYE SIFA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post