JAMAA WANNE WAKAMATWA KWA KUBAKA KENGE KWA ZAMU NA KUJIREKODI VIDEO YA NGONO


Wawindaji wanne wametiwa nguvuni na mamlaka ya uhifadhi wa misitu Nchini India Maharashtra, kwa tuhumza za kumbaka kenge kwa zamu (gang-raping).


Katika taarifa iliyotangazwa na Mamlaka hiyo imeeleza kuwa tukio hilo limebainika baada ya kufanya uchunguzi kwenye simu za wawindaji hao haramu (4), baada ya uchunguzi waliona Picha za Video wakifanya kitendo hicho ambacho kimepelekea watu walio wengi kukumbwa na mshangao.


Awali wawindaji hao walianza kutiliwa shaka na Mamlaka hiyo, ndipo wakaanza kufuatiliwa kupitia kamera maalum (cctv), zilizopo hifadhini humo.

Inaelezwa kuwa mara baada ya uchunguzi kukamilika watu hao watachukuliwa hatua za kisheria, ambapo kifungo cha juu zaidi kwa kosa hilo ikitajwa huwa ni miaka 7 gerezani.


Kenge aliyebakwa kwa zamu ni aina ya kenge wakubwa wanaojulikana kama bengal monitor lizards, ambao ni moja ya viumbe vinavyolindwa kwa sababu ya kuwa hatarini kutoweka katika uso wa dunia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post