VIVUTIO VYA UTALII VYA TANZANIA KUTANGAZA KUPITIA SHIRIKA LA NDEGE EMIRATES KUTAZAMWA NA ABIRIA WAPATAO MILIONI 90.2

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates, Badr Abbas kuhusu kuitumia ndege hizo katika kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ambapo ndege hizo husafirisha abiria milioni 90.2 kwa kila mwaka, Mazungumzo hayo yamefanyika leo katika makao makuu ya Shirika hilo lililopo katika Mji wa Dubai, Wa pili kulia ni Meneja wa Masoko wa Afrika wa Shirika hilo Muhamed Riz pamoja na Balozi mdogo wa Tanzania Dubai, Idd Bakari.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Afrika wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates, Badr Abbas jinsi vivutio vya utalii vya Tanzania vitajulikana klupitia ndege hizo kwani Emirates husafirisha abiria wapatao 90.2 kwa kila mwaka, Mazungumzo hayo yamefanyika leo katika makao makuu ya Shirika hilo lililopo katika Mji wa Dubai, Wa pili kulia ni Meneja wa Masoko wa Afrika wa Shirika hilo Muhamed Riz akiwa na Balozi Mdogo wa Dubai, Idd Bakari


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akimuonesha picha ya baadhi ya vivutio vya utalii vya Zanzibara Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Afrika wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates, Badr Abbas mara baada ya kuona picha ukutani ya Zanziba iliyowekwa katika Ofisi za makao makuu ya Shirika la ndege la Emirate , wa kwanza kulia ni Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai , Mhe. Idd Bakari



Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Afrika wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates, Badr Abbas kuhusu kuitumia ndege hizo katika kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania mara baada ya kufanyika kwa mkutano leo katika makao makuu ya Shirika hilo yaliyopo Dubai, Wa pili kulia na Meneja wa Masoko wa Afrika wa Shirika hilo.
Muhamed Riz akiwa na Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Idd Bakari


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Afrika wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates, Badr Abbas mara baada mkutano uliofanyika baina yao wa kutangaza vivutio vya utalii kupitia ndege za Emirates. Wa pili kulia na Meneja wa Masoko wa Afrika wa Shirika hiloMuhamed Riz akiwa na Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Bakari Iddy

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akikabidhiwa zawadi na Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Afrika wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates, Badr Abbas mara baada ya kufanyika mkutano wa kuitumia ndege za Shirika hilo katika kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ambapo ndege hizo hunasafirisha abiria wapatao 90.2 kwa kila mwaka,


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungmza na Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Afrika wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates, Badr Abbas mara baada ya kufanyika mkutano wa kuitumia ndege za Shirika hilo katika kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ambapo ndege hizo hunasafirisha abiria wapatao 90.2 kwa kila mwaka,


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Afrika wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates, Badr Abbas mara baada mkutano uliofanyika baina yao wa kutangaza vivutio vya utalii kupitia ndege za Emirates. Wa pili kushoto na Meneja wa Masoko wa Afrika wa Shirika hilo Muhamed Riz akiwa na Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Bakari Iddy


............................................................


Mwandishi Wetu, Dubai.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amefanya mazungumzo na Uongozi wa juu wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania ambapo vivutio hivyo vya utalii vitaweza kutazamwa na abiria wapatao milioni 90.2 ambao husafiri kila mwaka kwa kutumia ndege hizo



Aidha, Dkt.Ndumbaro amesema Tangazo hilo litakuwa likitazamwa na mamilioni ya abiria hao kila wakati ndege za Shirika hilo zitakapokuwa zikiruka (take off)


Dkt. Ndumbaro amebainisha hayo leo katika Mji wa Dubai alipokutana viongozi wa Shirika hilo ambalo mbali ya kusafirisha abiria milioni 90.2 duniani kote pia husafirisha abiria wapatao milioni 20 ambao huunganisha ndege nyingine


Katika hatua nyingine, Dkt.Ndumbaro amesema katika mazungumzo hayo wamekubaliana kutaandaliwa makala tano (Documentaries ) za kuelezea vivutio vya utalii vya Tanzania ikiwemo Zanzibar, Serengeti, Ngorongoro pamoja na Mlima Kilimanjaro

'' Shirila la ndege la Emirates ni Shirika kubwa sana Duniani lengo letu kama nchi ni kuhakikisha abiria wapatao milioni 90.2 wanaviangalia vivutio vyetu kisha wanavipenda halafu wanatembelea Tanzania'' amesisitiza Dkt. Ndumbaro



Katika mazungumzo hayo amesema Uongozi wa ndege hizo umeonesha utayari wa kushirikiana katika kuitangaza Tanzania kiutalii na ifika mwanzoni mwa mwezi wa tano mwaka huu wataingia makubaliano (MOU) baina ya Tanzania na Shirika hilo

Akifafanua mazungumzo hayo Dkt.Ndumbaro amesema kati ya abiria watakaoangalia vivutio wengi wao watavutiwa na hatimaye sehemu ya watu hao waweze kuja kutembelea Tanzania


" Shabaha yetu kubwa kama nchi ni kuhakikisha tunafikia watalii milioni 5 ifikapo mwaka 2025, Tunaamini tutalifikia lengo hilo" amesisitiza Dkt.Ndumbaro

Ameongeza kuwa Tanzania inategemea utalii wake wa Wanyamapori kwa asilimia 100 hivyo kupitia mkakati wa kutumia wa kutangaza vivutio vingine vya utalii kama vile utalii wa fukwe, utalii wa utamaduni pamoja na utalii wa ikolojia utaweza kujulikana dunia kote na kuwa chachu ya watalii wengi kuanza kumiminika nchini Tanzania.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Masoko wa Afrika wa Shirika la ndege la Umoja wa Falme za Kiarabu la Emirates, Badr Abbas amesema Shirika la Emirate lipo tayari kufanya kazi na Tanzania katika kuhakikisha vivutio vya utalii vya Tanzania vinajulikna pande zote za Dunia

'' Tutakapofikia makubaliano tutahakikisha pia matangazo ya vivutio vya Utalii wa Tanzania vinawekwa kwenye Tovuti pamoja na mitandao ya kijamii ikiwemo facebook, instagram pamoja na twitter ya Shirika hili ambayo imekuwa ikifuatiliwa na watu wengi Duniani,

Kwa upande wake, Balozi Mdogo wa Dubai, Mhe. Idd Bakari amesema mazungumzo yamekuwa na tija na hivyo kupitia Shirika hilo idadi ya watalii itaongezeka kupitia matangazo yatakayokuwa yakiruka wakati ndege za Shirika hilo zitapokuwa zikiruka

'' Mazungumzo haya baina yetu na Shirika la Emirates yataipaisha Tanzania vivutio vya utalii vitaweza kujulikana Duniani kote kuwa vipo Tanzania na hivyo watalii wengi watweza kuitembelea Tanzania

Katika mazungumzo hayo Ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro pamoja na Balozi Mdogo wa Tanzania, Mhe.Idd Bakari

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments