CHUO CHA TAIFA CHA UTALII CHAZINDUA MAFUNZO KWA WATOA HUDUMA KATIKA MNYORORO WA UTALII KUPITIA MRADI WA UVIKO-19 MWANZA


Mkuu wa Wilaya ya Magu Sallum Kali, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  Mhandisi Robert Gabliel katika uzinduzi wa mafunzo kwa watoa huduma za utalii Mkoani Mwanza kuhusu mwongozo wa kukabiliana na Uviko-19 katika Sekta ya utalii.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Dakitari Shogo Sedoyeka akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo kwa wadau wa Sekta ya utalii juu ya kukabiliana na Uviko-19 uliofanyika leo hii Jijini Mwanza
Watoa huduma katika mnyororo mzima wa utalii wakiwa kwenye uzinduzi wa mafunzo ya mwongozo wa kukabiliana na Uviko-19
Watoa huduma kutoka Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Mwanza wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jijini Mwanza
**

Na Hellen Mtereko, Mwanza

Chuo cha Taifa cha utalii kimezindua mafunzo kwa watoa huduma katika mnyororo wa utalii kupitia mradi wa Uviko-19 Mkoani Mwanza.

Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 kwenye ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Mafunzo hayo ya siku tano yamelenga kuwajengea uwezo watoa huduma za utalii juu ya namna bora ya kukabiliana na janga la Uviko-19, kwakuzinga matakwa ya kiafya,usalama pamoja na kuboresha huduma zinazotolewa ili kuimarisha ushindani katika masoko mbalimbali nchini.

Akizindua mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Magu Salum Kali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Uviko-19 awamu ya kwanza kupitia mpango wa maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko-19.

Amesema janga la Uviko-19 liliathiri kwa kiasi kikubwa Sekta ya utalii Duniani, kwaupande wa Tanzania idadi ya watalii ilipungua kutoka watalii milion 1,527,230 mwaka 2019 hadi kufikia watalii 620,867 kwa mwaka 2020 sawa na asilimia 59.3

"Tumeshudia kuyumba kwa biashara za utalii hasa kufungwa kwa baadhi ya makampuni ya utalii na hoteli lakini kwa sasa Sekta ya utalii Nchini imeanza kuimarika kutokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita ikiwemo hii ya kutoa mafunzo", amesema Kali.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Dk. Shogo Sedoyeka amesema kuwa Chuo hicho ni Taasisi iliyoko chini ya Wizara ya maliasili na utalii na wamepata fedha za Uviko ambazo zimewazesha kutoa mafunzo kwa wadau muhimu kwenye mnyororo wa utalii katika Mikoa 8 ya Tanzania bara.

"Mafunzo haya tumekwisha kuyatoa Mkoani Lindi,Mtwara,Ruvuma,Njombe,Iringa,Mbeya na leo tunamalizia Mkoani Mwanza na Mara, huku kwa Mkoa wa Mwanza tunarajia kutoa mafunzo kwa wadau wa utalii 150", amesema Sedoyeka.

Amesema pamoja na ugonjwa wa Uviko-19 kuendelea kuwepo ni lazima shughuli za uzalishaji katika Sekta ya utalii kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla ziendelee ili uchumi uzidi kuimarika.

Kwa upande wake msimamizi wa shughuli za kiutendaji katika Hotel ya Farms iliyoko Mkoani Mwanza, Shabani Myombe ambae ni mshiriki wa mafunzo hayo amesema kuwa mafunzo hayo yataongeza ufanisi katika kazi na yatawaondolea uoga pindi wanapokuwa wakitoahudumia kwa wateja wao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments