SHEREHE ZA ALAMA YA MWAKA MMOJA WA MAMA' RAIS SAMIA KUTIKISA SHINYANGA MJINI WEEKEND HIITaasisi ya Bega kwa Bega na Mama Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na akina mama wilaya ya Shinyanga Mjini wameandaa sherehe Maalumu ya Maadhimisho ya mwaka mmoja wa Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan madarakani. Sherehe hizi zitafanyika Mjini Shinyanga Machi 12 - 13 2022.

Katika Sherehe hizo Taasisi ya Bega kwa Bega na Mama Samia Suluhu Hassan imeandaa Matembezi Maalumu siku ya Jumamosi Machi 12,2022 yatakayoanzia Viwanja vya CCM Mkoa wa Shinyanga mpaka uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.

👉 Vile vile Taasisi hiyo imeandaa Semina kwa Wajasiriamali wadogo wadogo na Wamachinga, siku ya Jumapili Machi 13,2022 katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, watapewa Elimu juu ya umuhimu wa kupata Bima za Moto ili kulinda Mitaji yao na Majanga ya moto

Wote mnakaribishwa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments