COSTECH YAWANOA WAANDISHI WA HABARI MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI


Mkurugenzi Mkuu wa taasisi na usanifu wa mitambo Tanzania (TEMDO ) Mhandisi Fredrick Kahimba akiwa na mkurugenzi wa menejimenti ya maarifa  kutoka COSTECH Dr. Philbert   Luhunga pamoja na waandishi wa habari akielezea teknolojia zinazozalishwa katika taasisi hiyo Mara baada ya Waandishi kutembelea TEMDO kwa lengo la kujifunza  habari za matokeo ya utafiti.

*****

Rose Jackson,Arusha.

Tume ya sayansi na teknolojia Tanzania COSTECH imetoa mafunzo  ya siku nne kwa waandishi wa habari Mikoa ya Kanda yw Kaskazini na  watafiti  lengo likiwa ni kuhakikisha taarifa za utafiti na ubunifu  zinaandikwa kwa lugha rahisi ambayo itawafanya wananchi kuelewa.

Akizungumza katika semina ya mafunzo hayo inayofanyika jijini Arusha mkurugenzi wa menejimenti ya maarifa kutoka COSTECH  Dr Philbert Luhunga amesema kuwa kuna matokeo mengi ya utafiti ambayo wananchi Wanapaswa kuyaelewa kupitia waandishi.

Amesema kuwa waandishi wanapoandika habari za sayansi na matokeo ya  utafiti wataweza kuibadilisha jamii na kuleta mabadiliko kwenye jamii kwa kuwa wananchi watapata taarifa za utafiti ambazo zitaleta maendeleo endelevu.

"Tumekuwa na tafiti mbali mbali kutoka taasisi za  utafiti na tumeona Kuna matokeo mengi ya utafiti ambayo wananchi Wanapaswa kufahamu hivyo tunaamini kuwa waandishi wanapaswa kuandika habari hizi  ziwafikie wananchi kwa kuwa ndio walengwa wakubwa wa kujua matokeo ya tafiti hizo",alisema Dr.  Luhunga.

Aidha Dr Luhunga amewasihi wanahabari kuhakikisha wanaisemea  mazuri serikali kwa kuandika mema ,huku akiwataka waandishi kujiheshimu na kujitambua.

Akiwasilisha mada katika mafunzo hayo Dr Sigsbert Mmasi kutoka taasisi ya  usanifu wa mitambo Tanzania (Temdo) amesema kuwa taasisi hiyo imefanikiwa kubuni teknolojia mbali mbali ikiwemo mashine na vitendea kazi vya hospitalini ambavyo vimekuwa Ni mkombozi wa wananchi katika kurahisisha shughuli.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hao Noeli Urasa amesema kuwa anashukuru COSTECH kwa kutoa mafunzo hayo kwani yamempa uelewa wa kuandika habari za matokeo ya utafiti ambazo zitawezesha jamii kupata majawabu ya changamoto wanazokabiliana nazo.


 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments