Dunia Ina Mengi!!! KUTANA NA MZEE HUYU MWENYE UMRI WA MIAKA 339 NA YUPO HAI


Mambo duniani ni mengi aisee! Ni juu yako kuyapembua na kuyaamini au kutokuyaamini.

Hivi; ukiambiwa kuna mzee nchini Uturuki amegonga miaka 339 duniani utaamini?

Basi ishu iko hivyo; ila ukiamini utaungana na wenzako wasioamini na usipoamini utakuwa sehemu ya wasioamini kwani ndivyo ilivyo kwenye mitandao ya kijamii baada ya video ya mtu huyo kusambaa kwa kasi.

Katika ulimwengu wa mitandao ya kijamii video ya mtu huyo imekuwa agenda, wapo wanaosema haiwezekani mtu akaishi miaka yote hiyo, huku wengine wakisema inawezekana.

Hata hivyo, baada ya video hiyo kuwa gumzo ulimwenguni, jamaa mmoja alijitokeza kwenye mitandao ya kijamii na kujitambuliwa kuwa yeye ni ndugu wa kikongwe huyo na kufafanua kuwa ndugu yake hajafikisha miaka hiyo ila ametimu miaka 109.

Katika taarifa yake jamaa huyo aliongeza kuwa, ndugu yake siyo Mturuki bali ni Mthailandi na kutaka watu wamuamini.

Hata hiyo, kama ilivyo mtazamo wa wengi kuhusu video hiyo wapo pia waliopinga ufafanuzi wake huo na kusema jamaa ameutoa bila kuweka vielelezo thabiti na kwamba huenda ameficha taarifa kupunguza “uajabu” wa maisha ya ndugu yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments