WAHUNI WAVUNJA MAKABURI NA KUIBA MISALABA, NONDO...DC KALLI AAGIZA WASAKWE
*****
Mkuu wa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza Salum Kalli amekerwa na vitendo vya baadhi ya wananchi kuvunja makaburi na kutoa vyuma chakavu kama nondo na waya na kwenda kuuza.

Akiwa katika zoezi la Uzinduzi wa Anwani ya makazi Februari 20,2022  DC Kalli ameagiza kusakwa na kutiwa nguvuni kwa wanaojihusisha vitendo hivyo mara moja. 

DC Kalli amesema amesikitishwa na tabia hiyo isiyo na utu ndani yake na ameliagiza Jeshi la Polisi kuwasaka kwa udi na uvumba na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wanaojihusisha vitendo hivyo.


"Nimeagiza Jeshi la Polisi kuwashughulikia haraka na wafikishwe mahakamani na katika hili yeyote atakayehusika na tuhuma hizi sitokuwa na huruma hata kidogo, si uungwana hata kidogo kwenda kuwabughudhi wapendwa wetu waliotangulia mbele za haki",alisema DC Kalli.

DC Kalli amefikia hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko toka kwa wananchi kuwa Makaburi ya Ndugu zao yamekuwa yakivunjwa misalaba, na nondo kuchomolewa vilevile baadhi ya makaburi yametinduliwa na kuachwa yakiwa wazi au mianya mikubwa na huku yakiwa yameharibiwa.

Aidha ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza siku ya 26.02.2022 kwa ajili ya kufanya usafi katika makaburi hayo, ikiwa ni pamoja na kufyeka vichaka ambavyo vimekuwa ni maficho ya wahalifu.


‘KAZI IENDELEE’


Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge Jimbo la Magu
+255 716 094 601
dbubeshi@gmail.com

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments