RPC ILALA APONGEZWA KWA MAHUSIANO MAZURI NA JAMII

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam ACP Jumanne Muliro amempongeza Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Ilala ACP Debora  Magiligimba kwa mahusiano mazuri na jamii kutoka mkoa wa kipolisi IIala.

Kamanda Muliro ameyasema hayo katika makabidhiano ya Gari  aina ya Toyota Land cruiser leo tarehe 13/01/2022 katika kituo cha Polisi Kati Jijini Dar es salaam mara baada ya Gari hilo la Polisi kufanyiwa matengenezo na Kampuni ya Ulinzi ya Vital Force Securty.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala ACP Debora Magiligimba  ametoa shukrani zake kwa Mkurugenzi wa kampuni hiyo ya ulinzi Ndg. Mehboob Raza Abdukair ambaye ametumia zaid ya Tsh 6,000,000/= kugharamia matengenezo ya gari hilo.  

Naye Ndg. Mehboob Raza Abdukair amesema kuwa anajiskia furaha kuwa sehemu ya wadau wanaounga mkono juhudi za Jeshi la Polisi na maendeleo ya Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Samia Hassan na kuahidi ataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi Kadri ya uwezo wake.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments