ADC YATANGAZA KUSIMAMISHA MGOMBEA KITI CHA USPIKA



 
 Katibu Mkuu wa Chama cha ADC Taifa, Doyo Hassani Doyo
NA OSCAR ASSENGA, TANGA.

CHAMA cha Alliance Democratic Change (ADC) kimesema kwamba kitasimamisha mgombea wa kiti cha Uspika na Naibu Spika wa Bunge na tayari wamekwisha kutoa kalenda ya uchukuaji fomu ndani ya chama na taratibu zake kwa wanachama wao.

Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu wa Chama cha ADC Taifa, Doyo Hassani Doyo wakati akizungumza kuhusiana na namna walivyojipanga kusimamisha mgombea kwenye kiti hivho baada ya kupata taarifa ya nafasi hiyo kuwepo wazi.

Alisema kwamba chama hicho Januari 7 mwaka huu mchana walipokea taarifa kutoka kwa Katibu wa Bunge kuwaarifu kwamba kiti cha Spika na Naibu Spika wa Bunge kipo wazi na kila chama chenye usajili wa kudumu kama kipo tayari kushiriki kianze mchakato wa kupata wagombea .

Alisema tayari chama hicho kimetoka kwenye vikao vya kikatiba na sasa wamekubaliana kusimamisha mgombea na ndio maana wametoa kalenda ya uchukuaji fomu ndani ya chama na taratibu zake ili wanachama wa ADC waweze kupata fursa hiyo na watanzania kwa ujumla ambao wanauwezo wa kuwa spika na naibu spika wa Bunge.

“Ratiba yetu sisi tumeanza Januari 12 mwezi huu hadi Januari 18 mwezi huo kwa ajili ya kuchukua foimu na kurejesha na taratibu za kawaida za kikanuni ikiwemo ada ya fomu 100,000 kwa ajili ya mgombea”Alisema Katibu huyo.

Hata hivyo alisema taratibu za chama wagombea wanatakiwa wapeleke CV ili waweze kuona mgombea anayegombea anasifa gani za kielimu ili waweze kuainisha sifa za mgombea kwenye taratibu wakati wanapeleka barua yao kwa spika kwenda kuwatambulisha wagombea wao .

Katibu huyo alisema kwamba wao wamejipanga kuweza kuleta ushindani na iwapo wabunge wataona mgombea wao ana sifa za kuwa spika na wanaomba wamchague ili aweze kuwa spika wa bunge hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments