RATIBA YA MAZISHI YA MIILI YA WAANDISHI WA HABARI WALIOFARIKI KWA AJALITaarifa ya kusafirishwa kwa miili ya waandishi wenzetu. 

Ndugu waandishi wa habari na wadau wa habari ifuatayo ni taarifa fupi baada ya kuaga miili ya wenzetu toka uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.


1. Mazishi ya Mwili wa Husna Mlanzi yamefanyika leo Jijini Mwanza yakihudhuriwa na Waziri wa Habari, MAwasiliano na Teknolojia Nape Nnauye

2. Mwili wa Antony Chuwa utasafirishwa kwa gari kwenda Moshi. 

3. Mwili wa Johari utasafirishwa kwa gari kwenda Arusha. 

4. Mwili wa Abel Ngapemba utasafirishwa kwa ndege kwenda Dar es Salaam; na 

5. Mwili wa Steven Msengi umesafirishwa kwenda Dar es Salaam  usiku huukwa gari.

Taarifa nyingine za mazishi ya hao ndugu zetu tutawajukisha kesho.

Tuzidi kuwaombea wenzetu. 

 Edwin Soko 
 Mwenyekiti 
 Mwanza Press Club 
 12. 01.2022

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments