MTATURU ASISITIZA VIPAUMBELE MFUKO WA JIMBO



............................................................

KAMATI ya mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo imeketi chini ya mwenyekiti wake Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu na kugawanya fedha kiasi cha Sh Milioni 44,024,000 ikiwa ni mgao kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Akimkaribisha mwenyekiti kwa ajili ya kufungua kikao, katibu wa mfuko ambaye ni afisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi Joyce Emmanuel amemshukuru mbunge huyo kwa utayari wa kuitisha kikao mapema na kusoma maombi yanayofikia Sh Milioni 157 yaliyoletwa kutoka kwenye vijiji na kata mbalimbali.

Baada ya kupokea taarifa hiyo Mh Mtaturu kabla ya kufungua kikao aliwaomba wajumbe wayapitie maombi kwa kina na kupitisha vipaumbele ili kuunga mkono juhudi za wananchi kwenye miradi yao.

“Ndugu zangu miradi tuliyoiunga mkono mwaka wa fedha wa 2020/20 21 imeonyesha tija na kuna maeneo tayari imeanza kutoa huduma,niwasihi wajumbe na mratibu wa mfuko kufuatilia utekelezaji wa miradi hii ili ilete tija kwa wananchi,”alisema.

Amewaahidi wajumbe kuendelea kuibana serikali kutenga fedha zaidi za miradi kwenye jimbo na wilaya.

Wakizungumza katika kikao hicho baadhi ya wajumbe wameshauri miradi iliyoanzishwa na nguvu za wananchi iungwe mkono kupitia fedha hizo ili iwe chachu kwenye jamii.

“Tunakupongeza Mh Mbunge kwa juhudi zako ukiwa bungeni kuomba fedha ambazo zinatekeleza miradi mingi jimboni kwa sekta za elimu, afya, Maji, umeme na barabara,”alisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments