AWAMU YA SITA YANG'ARISHA SINGIDA MASHARIKI


............................................

ZOEZI la Uchimbaji wa visima virefu katika Jimbo la Singida Mashariki linaendelea ambapo kwa sasa ni zamu ya Kijiji Cha Mbwanjiki Kata ya Ikungi.

Kazi hiyo inafanywa na Mkandarasi M/s Target na ameshachimba mita zipatazo 152 na kupelekea maji mengi kupatikana na hivyo kufanya visima vilivyokamilika kuchimbwa kufikia vinne katika vijiji vya Kimbwi, Ujaire na Msule.

Mradi huo wa visima unatarajiwa kukamilishwa kwenye vijiji vya Mapando, Damankia na Mang'onyi ambapo baada ya kupatikana vyanzo vya maji hatua inayofuata ni kujenga miundombinu ili wananchi waweze kupata maji safi na salama.

Matokeo hayo ni jitihada za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan iliyoahidi kusogeza huduma za maji karibu na wananchi ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),iliyoahidi kumtua mama ndoo ya maji kichwani.

Kwa sasa wilaya ya Ikungi inatoa maji safi na salama kwa asilimia 58 lakini baada ya kukamilika kwa miradi hii upatikanaji wa maji utafikia asilimia 73.

Akizungumza na mtandao huu Mbunge wa Jimbo hilo Miraji Mtaturu ameishukuru serikali kwa kutenga fedha Ili kutekeleza miradi hiyo ya maji.

"Tunamshukuru Rais wetu Mh Samia Suluhu Hassan kwa kusimama imara kuitekeleza Ilani tuliyoinadi wakati wa kampeni,hii ni hatua kubwa inayoleta matumaini na uhakika wa wananchi wetu kupata maji,kweli anaposema Kazi Iendelee anamaanisha kwa vitendo,"alisema Mtaturu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post