SPIKA NDUGAI AMUOMBA RADHI RAIS SAMIA,ASIKITISHWA NA KAULI YAKE YA KUMVUNJA MOYO


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai,akisisitiza jambo kwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Januari 3,2022 jijini Dodoma .

Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 blog-DODOMA.

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amemomba radhi Rais Samia Suluhu Hassan na watanzania kwa ujumla kwa namna yoyote ambayo alihisiwa kutoa maneno ya kumvuja moyo na kusababisha Rais kuvunjika moyo.

Ndugai amesema hayo mapema leo Bungeni Jijini Dodoma katika Mkutano wake na waandishi wa habari uliolenga mambo kadhaa ikiwemo kuomba radhi kwa kauli yake aliyoitoa mwishoni mwa mwaka 2021 ikieleza kukerwa na madeni ambayo Tanzania inakopa kwenye Benki ya IMF.

Amesema kauli aliyoitoa ni tofauti na baadhi ya vyombo vya habari vilivyo mnukuu na kudai kwamba amechezewa
 na mitandao ya kijamii na hakuwa na nia mbaya kama ambavyo imeeleweka na kusababisha taharuki kwa jamii.

Hatua hiyo imekuja kufuatia  video ambayo Spika Ndugai anaonekana akipinga utaratibu wa Serikali wa uchukuaji mikopo kutoka taasisi za fedha na kwamba kwa mwendo huo nchi itakuja kupigwa mnada.

Video hiyo iliyozua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii na kupewa uzito mkubwa na vyombo vya habari nchini imepelekea  Spika Ndugai kukiri wazi kwamba amekosea na amaomba msamaha Kwa Rais,wananchi na Kwa Mwenyezi Mungu.

'Kwa wale wote waliokwazwa na kauli yangu naomba sana mnisamehe,nimekosea sana , kwani natambua kazi kubwa iliyofanywa na Rais Samia katika kipindi kifupi cha uongozi wake,mengi ameyafanya kwenye Wilaya yangu ,

Mfano  mkopo wa sh. trilioni 1.3 ambazo Tanzania imepata kutoka IMF, fedha hizo zimefanya mambo makubwa hasa katika Wilaya ya Kongwa ambayo imepata mgawo wa sh. bilioni 3 sawa na mapato yake ya ndani ya mwaka mmoja kwa ajili ya ujenzi wa madarasa,"Amesema 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments