Breaking

Post Top Ad

https://refpasrasw.world/L?tag=d_1066073m_7669c_&site=1066073&ad=7669

Monday, January 3, 2022

SIMBA SC WAZINDUA JEZI MPYA TENA...KUANZA KUTUMIKA MAPINDUZI CUPKlabu ya Simba imezindua jezi zao mpya leo Jumatatu, Januari 3, 2022, kuelekea mchezo wao katika Michuano ya Mapinduzi Cup.

Jezi hizo zimezinduliwa visiwani Zanzibar na Afisa Habari wa Klabu hiyo Ahmed Ally, na zitatumika katika michuano ya Mapinduzi Cup na Kombe la Azam Sports (ASFC).

Kwa sasa Jezi hizo zinapatikana madukani yote ya Vunja Bei, Afisa habari huyo amewaomba wanasimba kujipatia jezi mapema.

Akizungumzia uzinduzi huo, Afisa Habari Simba SC, Ahmed Ally amesema; “Tumezindua jezi mpya ambazo tutaanza kuzitumia kwenye michuano ya Mapinduzi hapa Zanzibar, pia tutazitumia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

“Mashabiki wanaweza kununua jezi zetu mpya kwa ajili ya klabu yao, imekua ni kawaida yetu kufanya jambo hili na wengine wamekua wakituiga…”

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages