PASTA AZINDUA 'CHUPI NA SIDIRIA ZA UPAKO' ZENYE SURA YAKE KUSAIDIA WANAWAKE WAOLEWE


Pasta Dr J.S. Yusuf wa Kanisa la Touch for Recovery Outreach International mjini Abuja nchini Nigeria amezindua nguo za ndani na sidiria zenye chapa ya picha yake ili kuwasaidia wanawake waseja 'singo' wanaotamani kuolewa kuwavizia waume zao.

Kwa mujibu wa pasta Dr J.S. Yusuf, aliagizwa na Mungu kuzindua chupi hizo za ‘baraka’ ili kufungua milango ya ndoa Mwaka Mpya.

Mchungaji huyo alinukuu mstari kwenye kitabu cha Hesabu 23:20 unaosema“Tazama nimepokea amri ya kubariki, naye amebariki, wala siwezi kubadili.”

Chupi hizo zinasemekana pia kuwasaidia wanawake kujikinga na magonjwa na kupata bahati njema wakiwa na wanaume.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post