ASKARI POLISI AFARIKI AKIJIBURUDISHA NA MREMBO GESTI


Polisi wameanzisha uchunguzi katika kisa ambapo mwanaume mmoja amefariki katika chumba cha hoteli mjini Ndhiwa Kaunti ya Homa Bay nchini Kenya baada ya kufurahia burudani kati yake na mwanamke mmoja.

Kamanda wa polisi katika Kaunti Ndogo ya Ndhiwa Paul Rioba alisema kuwa kisa hicho kilitokea usiku wa Ijumaa, Januari 21, na mwanaume ambaye jina lake haliwezi kutajwa alikuwa afisa wa polisi.

 Mwanaume huyo anaripotiwa kuzimia na kufariki wakati wa kushiriki tendo la ndoa na mwanamke ambaye polisi wamethibitisha kuwa na umri wa miaka 25. Kwa mujibu wa polisi, mwanaume huyo alikuwa na umri wa miaka 55.

“Mwanaume huyo alifariki akiwa chumbani na mwanamke huyo. Kwa mujibu wa mwanamke huyo ambaye tunamzuilia, mwanaume huyo alizimia na kuaga dunia wakati wa tendo la ndoa,” Rioba alisema.

Mwanaume huyo anasemekana kuwasili wa kwanza na kulipia chumba chao cha hoteli huku mwanamke huyo akijiunga naye baadaye. 

Katika taarifa aliyoandikisha na polisi, mwanamke huyo alisema kuwa mwanaume huyo alipozimia hakuwa na budi ila kuarifu usimamizi wa hoteli na ndipo hapo maafisa wa polisi walipoarifiwa kuhusu tukio hilo na mwanamke huyo kutiwa mbaroni.

 “Ametiwa mbaroni anapoendelea kusaidia polisi katika uchunguzi. Hatutaki kuotea chochote kwa sasa hadi pale ambapo upasuaji wa mwili utafanywa ili tubaini kilichojiri,” Rioba alisema.

 Mwili wa marehemu ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Manyatta Kabodo ukisubiri kufanyiwa upasuaji.

Chanzo-  Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post