ALIYEGOMBANA NA MKEWE AJIUA KWA MKANDA BAADA YA KUDHIBITIWA ASIWACHINJE WATOTO

Daud Samwel (30) mkazi wa Kitongoji cha Burunga Wilaya ya Serengeti mkoani Mara amejinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali yake baada ya kudhibitiwa kuwachinja watoto wake wanne kufuatia mke kumkimbia baada ya kuzidiwa na kipigo.

Tukio hilo limethitibitishwa na Polisi wilaya ya Serengeti Mganga aliyefanya uchunguzi na Mwenyekiti wa kitongoji linadaiwa kutokea kati ya Januari 24 usiku mwili wake uliokuwa umening’inia kwenye mti jirani na kwake umegunduliwa na majira Januari 25 asubuhi wanapita na kutoa taarifa polisi.

Albert Mnalimi Mganga kutoka Hospitali ya Nyerere aliyefanya uchunguzi wa mwili amesema chanzo cha kifo chake ni kubana mishipa ya shingo na kukata pumzi.

”Kwa kuwa alibana shingo kwa mkanda ile ya maturubai na Oksijeni ikashindwa kwenda kwenye ubongo na kusababisha kifo,hakuwa na jeraha sehemu nyingine,”amesema.

Mbabaji Aloyce jirani yake amesema,kabla ya uamuzi huo alimpiga sana mke wake na kulazimika kukimbia.

”Januari 24 saa 2 usiku alinigongea nikamfungulia akaniambia kuwa mke wake amekimbia nimpe simu ampigie nikampa wakati huo sikujua ana panga,”amesema.

“Katika maongezi yake kwenye simu akasema,kwa kuwa umekimbia sasa naenda kuchinja mtoto mmoja mmoja tuone kama hutokuja kuwaona,kwa kuwa alikuwa amelewa gongo na inasadikika alikuwa anavuta bangi nikalazimika kumbana asiende kufanya unyama huo akawa mkali sana,”amedai.

Amesema,alilazimika kujitosa kumdhibiti wakavurugana na kuanguka chini akajaribu kuchomoa panga akambana ili asimkate na watu wakajitokeza wakafanikiwa kumpora panga,hata hivyo aliendelea kubainisha adhima yake lazima aue.

“Nililazimika kumpigia simu Ocd na balozi akataarifiwa,polisi hawakuchukua muda wakawa wamefika kwake hakuonekana ikawalazimu kuondoka na watoto na mama yao kwa ajili ya usalama wao,asubuhi nimeondoka bila kujua chochote baadae naambiwa kafa kwa kujinyonga,”amesema.

Mwenyekiti wa Kitongoji John Magoto amesema kuwa mara kwa mara alikuwa akipokea malalamiko ya mke wa Daud kwa jinsi alivyokuwa akimpiga hasa anapokuwa amekunywa pombe.

“Mara ya mwisho alimpiga sana mke wake mpaka akazimia baada ya kumkatalia kuwa ataacha kutembeza nyanya kwa ajili ya mahitaji ya familia kwa madai kuwa fedha anazopata zinampa kiburi,alitoroka na kwenda Dutwa kwenye machimbo,amerudi hivi karibuni na kuanza migogoro na hatimaye kafikia kujiua,”amesema.

Amesema taratibu za mazishi zinasubiri wazazi wake ambao wanadaiwa wanaishi Kenya,mwili kwa sasa umehifadhiwa nyumbani kwake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post