SIMBACHAWENE : SILAHA 228 ZASALIMISHWA AGIZO LA RAIS SAMIA

 

Na Dotto Kwilasa - Malunde 1 blog, Dodoma

KUTOKANA na agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kutaka wamiliki wa silaha kinyume na Sheria kuzisalimisha, jumla ya silaha  228 zimesalimishwa kwa Jeshi la Polisi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema hayo  leo Desemba 6,2021,wakati akiongea na waandishi wa habari  kuhusu  utekelezaji wa tangazo la msamaha kwa usalimishaji wa silaha haramu tarehe 1/11/2021 hadi tarehe 30/11/2021.

Waziri Simbachawene amesema Jumla ya silaha zilizosalimishwa ni 228 huku akilitaka  Jeshi hilo  kuangalia upya uwezekano wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Silaha na Risasi ya Mwaka 2015.


"Kwa mchanganuo wa Pistol 05 sawa na 2.2% ya silaha zote zilizosamilishwa, magobore 174 sawa na 76.3% ya silaha zote zilizosalimishwa, S/gun 38 sawa na 16.7% ya silaha zote zilizosalimishwa, Rifle 10 sawa na 4.4% ya silaha zilizosalimishwa   na SMG 01 sawa na 0.4% ya silaha zote zilizosalimishwa,”amesema.


Amesema kufanya hivyo ni   ili kuweka utaratibu wa kisheria wa kutengeneza  na kuruhusu Magobore kwa kuwa silaha hizo zimekuwa zikitumika kwa shughuli za ulinzi katika jamii.


Pia imesalimishwa jumla ya mitutu 12 ambapo mitutu 11 imesalimishwa Mkoa wa  Tanga na Mtutu 01 umesalimishwa  Mkoa wa Mbeya.

“Kati ya silaha zilizosalimishwa imeonekana kuwa magobore ni asilimia 76.3 jambo linaloonesha kuwa tatizo la utengenezaji wa silaha za kienyeji  yakiwemo magobore ni kubwa hapa nchini,”amesema.


Amesema kufuatia matokeo haya ya usalimishaji wa silaha haramu,Waziri Simbachawene amelielekeza  Jeshi la Polisi kuangalia upya uwezekano wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Silaha na Risasi ya Mwaka 2015 ili kuweka utaratibu wa kisheria wa kutengeneza  na kuruhusu Magobole kwa kuwa silaha hizo zimekuwa zikitumika kwa shughuli za Ulinzi katika jamii.


Pia,kufanya misako kwa kutumia taarifa za kiintelelijensia ili  kuwabaini na  kuwakamata wale wote wanaomiliki silaha kinyume na Sheria na kisha kuwachukulia hatua za kisheria.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments