MSHINDI MWINGINE WA KAMPENI YA SIMBANKING “MZIGO PROMOSHENI” YA BENKI YA CRDB APATIKANA, AONDOKA NA TOYOTA IST - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Thursday, December 23, 2021

MSHINDI MWINGINE WA KAMPENI YA SIMBANKING “MZIGO PROMOSHENI” YA BENKI YA CRDB APATIKANA, AONDOKA NA TOYOTA IST

Mkurugenzi Wa Hazina wa Benki ya CRDB, Alex Ngusaru (kulia) akimkabidhi kadi ya gari Mshindi wa Kampeni ya Simbanking “Mzigo Promosheni” Kwa Mwezi Novemba 2021, Victor Danford Mbulingwe mkazi wa Dar es salaam kupitia Tawi la Benki ya CRDB Kijitonyama aliyeondoka na gari aina ya Toyota IST, ambaye ameongoza kwa kufanya miamala mingi zaidi kwa kipindi cha mwezi Novemba. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo katika Tawi la Benki hiyo, Kijitonyama Dar Es Salaam. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili, Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Kijitonyama, Rosemary Nchimbi pamoja na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd.
katika kampeni hiyo ya “Mzigo Promosheni” Benki ya CRDB imemekuwa ikiwazawadia wateja kutokana na miamala wanayoifanya kupitia SimBanking, na mpaka sasa wameshatoa zaidi ya zaidi ya shilingi milioni 15 kwa wateja zaidi ya 500 wanaoongoza kwa idadi ya miamala kila siku. Lakini pia wamekuwa na washindi wanaoongoza kwa idadi ya miamala kila mwezi ambao wao wamekuwa wakijishindia gari aina ya Toyota IST. Jumla ya washidhi sita wa gari wamepatikana kutoka mikoa mitano nchini, ambao ni Mshindi wetu wa mwezi Juni, Kevin Ngao (Dar es salaam), Mshindi wa mwezi Julai, Madina Ramadhani (Dodoma), Mshindi wa mwezi Agosti, Afande Hamadi Juma Pole (Mwanza), Mshindi wa mwezi Septemba, Rajabu Daniel Msuya (Tanga), Mshindi wa mwezi Oktoba, Elisha Edison Mwamahonje (Mtwara) pamoja na Victor Danford Mbulingwe ambaye ni mshindi wa kampeni hiyo kwa mwezi wa Novemba.

Mkurugenzi Wa Hazina wa Benki ya CRDB, Alex Ngusaru (kulia) akimpongeza Mshindi wa Gari aina ya Toyota IST kupitia Kampeni ya Simbanking “Mzigo Promosheni” kwa Mwezi Novemba 2021, Victor Danford Mbulingwe (kushoto) mkazi wa Dar es salaam kupitia Tawi la Benki ya CRDB Kijitonyama, ambaye ameongoza kwa kufanya miamala mingi zaidi kwa kipindi cha mwezi Novemba.
Mkurugenzi Wa Hazina wa Benki ya CRDB, Alex Ngusaru akizungumza katika hafla ya kumkabidhi gari Mshindi wa Kampeni ya Simbanking “Mzigo Promosheni” kwa Mwezi Novemba 2021, iliyofanyika leo katika Tawi la Benki ya CRDB,Kijitonyama Dar Es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili akilelezea kwa waandishi wa habari namna Kampeni ya Simbanking “Mzigo Promosheni” kwa Mwezi Novemba 2021 ilivyoendeshwa na mpaka kupatikana mshindi wa Gari aina ya Toyota IST.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd akizungumza.Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages