DEREVA ALIYESABABISHA AJALI ILIYOUA POLISI AHUKUMIWA MIAKA MINNE JELA
Wednesday, December 01, 2021
Na Amiri Kilagalila,Njombe
ALIYEKUWA dereva wa basi la Sharon lililosababisha ajali na kusababisha vifo vya askari wanne wa Jeshi la Polisi mkoani Njombe na majeruhi saba, William Emmanuel (28)ahukukumiwa kifungo cha miaka minne jela na kufungiwa leseni yake kwa muda wa miaka miwili.
Akisoma hukumu hiyo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Njombe Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Liad Shamshama akiwa na Wakili wa Serikali Andrew Mandwa amesema tukio hilo la ajali lilitokea Februari 2020 maeneo ya mlima wa polisi barabara kuu ya Njombe Songea saa 12 alfajiri.
Amesema siku ya tukio dereva huyo alikuwa akiendesha basi aina ya Youtong hivyo alipofika maeneo ya mlima wa polisi alilipita gari lingine sehemu ambayo haikutakiwa kufanya hivyo.Akiwa kwenye mwendo mkali dereva huyo aliligonga gari la polisi aina ya Land cruiser na kusababisha vifo vya askari hao.
"Pamoja na kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka minne gerezani mshtakiwa pia amefungiwa leseni yake kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia leo,"amesema Shamshama.Askari waliofariki kutokana na ajali hiyo ni Marianus Hamis Saidi,Heri Athumani Soka, Michael Ernest Mwandu na Dickson Kagoda Maijo.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin