DC JASINTA MBONEKO AKABIDHI ZAWADI ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA 2022 KWA WAZEE KOLANDOTO


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) akikabidhi Mbuzi kwa ajili ya Sikukuu ya Krismasi/Mwaka Mpya kwa wazee wa kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza cha Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Elisha Robert akifuatiwa Afisa Utumishi wa Manispaa ya Shinyanga Getrude Gisena.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amekabidhi zawadi ya vyakula na mahitaji mbalimbali vyenye thamani ya shilingi 1,109,000/= katika kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza cha Kolandoto Manispaa ya Shinyanga ili kusherehekea Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2022.

Zawadi hizo ukiwemo mchele,mafuta ya kupikia,sabuni,juisi,biskuti,kuku,mbuzi,dawa za meno,sukari,mafuta ya kujipaka na viungo vya chakula vimetolewa na Kikundi cha wanawake maarufu ‘Soul Sisiters’ ambapo Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ni mwanachama na zawadi zingine zikitolewa na Uongozi wa Manispaa ya Shinyanga.

Mboneko amekabidhi zawadi hizo leo Alhamisi Desemba 23,2021 katika kituo hicho akiwa ameambatana na maafisa mbalimbali wa wilaya na Manispaa ya Shinyanga akiwemo Afisa Utumishi wa Manispaa hiyo Getrude Gisena.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo, Mboneko amesema serikali inajali na kuwapenda wazee hivyo itaendelea kuwahudumia na kuwatunza.

“Serikali yetu chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan inawajali wazee, inawapenda wazee na inawapenda watu wote. Lakini pia niwafikishie salamu za Mkuu wetu wa Mkoa Mhe. Sophia Mjema na yeye nilimwambia nakuja kuwatembelea wazee akasema wape salamu. Nimefurahi kuwaona wote mpo na nyuso nzuri, tunamshukuru Mwenyezi Mungu!, panapo uhai na sisi ni wazee watarajiwa hivyo tuna kila sababu ya kuwalinda na kuwatunza wazee wetu”,amesema Mboneko.


“Tunaishukuru sana serikali yetu chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kukilea kituo hiki cha Wazee Kolandoto na vituo vingine vilivyopo nchini na tutaendelea kusukuma mahitaji yote yanayohitajika kwa ajili ya kituo hiki ili kiendelee kuwahudumia wazee wetu na kwa namna yoyote ile hamtakiwi kuwa wanyonge kwa sababu sisi viongozi tunawapenda, tunawajali na tutaendelea kuwajali kwani wanahitaji upendo wa karibu”,ameongeza Mboneko.


“Lengo langu kuu la kuja hapa na wenzangu ni kuwasilisha zawadi hizi kwa niaba ya kikundi chetu na wenzangu niliosoma nao Chuo Kikuu kinaitwa Soul Sisters ambacho hutoa sadaka kila mwaka kwa ajili ya watu wenye mahitaji na mara nyingi huwa wanafanya sana kwa Dar es salaam. Kipindi hiki wakasema wewe (Jasinta Mboneko) mwanachama mwenzetu tuchagulie wapi tukasaidie na mimi nikawaambia tupeleke kwa wazee wangu wa Kolandoto na wenyewe wakafurahi”,ameeleza Mboneko.

Mboneko amezitaja zawadi zilizotolewa na Kikundi cha Soul Sisters kuwa ni mchele kilo 100, sukari kilo 50,mafuta ya kujipaka katoni moja na nusu,sabuni za unga pakti 60,sabuni za miche boksi 1,juisi katoni 4,biskuti boksi 2,dawa za meno katoni moja na nusu na kuku 6 huku Manispaa ya Shinyanga ikitoa mchele kilo 100, juisi katoni 4,mafuta ya kupikia lita 10,viungo vya kupikia chakula,nyama kilo 8 na mbuzi mmoja vyote vikiwa na thamani ya shilingi 1,109,000/=.

Mkuu huyo wa Wilaya amemtaka msimamizi wa kituo cha Kolandoto, Sophia Kang’ombe kuhakikisha vitu vilivyotolewa vinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa kwa walengwa husika.

Kwa upande wake, Msimamizi wa kituo hicho, Sophia Kang’ombe ameshukuru kwa msaada huo ambao umeongeza furaha kwa wazee hao.

Amesema hadi sasa kituo cha Kolandoto kina wazee 16 kati yao wanaume ni 12 na wanawake ni wanne.

Nao wazee hao akiwemo Zengo Masemba, Juakali Mihangwa na Limi Ngelela wamemshukuru Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Soul Sisters na wadau wengine kwa kuwapatia msaada huo kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya 2022.


ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akiwa amepiga magoti akiwasalimia wazee alipowasili  kwa ajili ya kukabidhi zawadi ya vyakula na mahitaji mbalimbali katika kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza cha Kolandoto Manispaa ya Shinyanga ili kusherehekea Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2022 leo Alhamis Desemba 23,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza cha Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni Afisa Utumishi wa Manispaa ya Shinyanga Getrude Gisena, kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii ambaye ni Msimamizi wa Kituo cha Wazee Kolandoto, Sophia Kang'ombe.
Sehemu ya wazee wa kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza cha Kolandoto Manispaa ya Shinyanga wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza na wazee katika kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza cha Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) akikabidhi Mbuzi kwa ajili ya Sikukuu ya Krismasi/Mwaka Mpya kwa wazee wa kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza cha Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Elisha Robert akifuatiwa Afisa Utumishi wa Manispaa ya Shinyanga Getrude Gisena.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) akikabidhi Mbuzi kwa ajili ya Sikukuu ya Krismasi/Mwaka Mpya kwa wazee wa kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza cha Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) akikabidhi dawa za meno kwa wazee wa kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza cha Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) , Afisa Utumishi wa Manispaa hiyo Getrude Gisena (kulia) wakifurahia jambo na wazee wakati wakikabidhi viungo vya chakula na zawadi mbalimbali kwa ajili ya Sikukuu ya Krismasi/Mwaka Mpya kwa wazee wa kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza cha Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) akifurahia jambo na wazee wakati akikabidhi viungo vya chakula kwa ajili ya Sikukuu ya Krismasi/Mwaka Mpya kwa wazee wa kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza cha Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza na wazee baada ya kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya kwa wazee wa kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza cha Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. 
 Zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya kwa wazee wa kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza cha Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. 
Mbuzi wa Sikukuu ya Krismasi/Mwaka Mpya kwa wazee wa kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza cha Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. 
 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja na wazee baada ya kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya kwa wazee wa kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza cha Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja na wazee na wadau wengine baada ya kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya kwa wazee wa kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza cha Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja na wazee na wadau wengine baada ya kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya kwa wazee wa kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza cha Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja na wazee na wadau wengine baada ya kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya kwa wazee wa kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza cha Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. 
 Mzee Juakali Mihangwa akitoa neno la shukrani kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Soul Sisters na wadau wengine kwa kuwapatia zawadi ya Sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya 2022.
Mzee Zengo Masemba akitoa neno la shukrani kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Soul Sisters na wadau wengine kwa kuwapatia zawadi ya Sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya 2022.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akipiga stori na wazee baada ya kukabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya kwa wazee wa kituo cha kulelea wazee na watu wasiojiweza cha Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. 

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments