MKE AMUUA MUMEWE KWA KUMCHOMA MOTO SINGIDA


Mwalimu wa Sekondari ya New Kiomboi mkoani Singida, Simon Roman (33) amefariki dunia baada ya kuchomwa moto na mkewe sababu ikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Tukio hilo lilitokea Desemba 27, 2021 jioni baada ya mume kurudi kutoka matembezi huku mkewe akitaka kujua kuhusu uhusiano wa mumewe na mmoja wa wanawake katika eneo hilo.


Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa Singida, Stella Mutabihirwa amemtaja mtuhumiwa wa mauaji ambaye ni fundi cherehani naye amelazwa hospitali ya mkoa wa Singida akipatiwa matibabu kutokana na majeraha ya moto aliyoyapata.

Mbali na mtuhumiwa, watoto wao Clara Anthony na Wisley Anthony wamelazwa hospitalini kwa majeraha ya moto huku Apolinary Simon (18) ambaye ni mdogo wa marehemu inadaiwa hali mbaya baada ya kuungua zaidi usoni.

Katika taarifa aliyoisambaza kwa vyombo vya habari, Kamanda Mutabihirwa amesema chanzo cha ugomvi ni mwanamke huyo kumtuhumu mumewe (marehemu) kwamba alikuwa na uhusiano na mwanamke mwingine jambo lililozua ugomvi kwa wawili hao.

“Majibizano yalipoendelea, mwanamke alikwenda kuchukua maji ya moto yaliyochemshwa kwa ajili ya kuoga akamwagia mumewe wakiwa sebuleni na kabla hajajua la kufanya alimwagia tena mafuta ya petroli kisha akawasha moto wa kiberiti,” anasema Kamanda Mutabihirwa.


Amesema moto huo ulisambaa ndani na kuunguza vitu vingi na kujeruhi wanafamilia waliokuwa ndani ya nyumba hiyo hivyo kusababisha hasara kubwa ambayo haijaweza kufahamika mara moja lakini Mwalimu huyo anajatwa kuwa aliungua vibaya mwili mzima.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments