RAIS SAMIA ATUMA ZA POLE KIFO CHA MCHUNGAJI GEHAZ JAPHET MALASUSA - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Wednesday, December 15, 2021

RAIS SAMIA ATUMA ZA POLE KIFO CHA MCHUNGAJI GEHAZ JAPHET MALASUSA


Rais Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dr. Alex Malasusa kufuatia kifo cha baba yake mzazi, Mchungaji Gehaz Japhet Malasusa.


Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Rais Samia amesema amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo hicho na kutoa salamu za pole kwa familia ya askofu huyo, ndugu, jamaa na marafiki na kumuombea kwa Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.


Mzee Malasusa alifariki dunia usiku wa kuamkia Desemba 8, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa anapatiwa matibabu.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages