Picha : MISA TANZANIA YAKUTANA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI KUCHOCHEA UWAZI, HAKI NA DEMOKRASIA

Mwandishi wa Habari Mwandamizi nchini Tanzania Jenerali Ulimwengu akizungumza wakati wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Sahara (Media Institute of Southern Africa - MISA Tanzania) imeendesha Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.

Mjadala huo umefanyika leo Jumatano Desemba 15,2021 jijini Dodoma ukiwa na lengo la kuwajengea uelewa wamiliki wa vyombo vya habari kuhusu kazi ya vyombo vya habari kwenye kuchochea uwazi, haki na demokrasia.

Lengo jingine la mjadala huo ulioongozwa na Waandishi wa Habari Waandamizi nchini Jesse Kwayu na Jenerali Ulimwengu ni kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoathiri uhuru wa kiuhariri unaosababisha kutokuwepo kwa uhuru wa kiuhariri kwenye vyombo vya habari unapelekea vyombo vya habari kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kusaidia jamii.

Mwandishi Mwandamizi nchini, Jenerali Ulimwengu  amesisitiza kuwa utawala wowote unaokandamiza uhuru wa vyombo vya habari unatoa mwanya wa maovu, ikiwemo rushwa na wizi wa mali za umma.

“Bila vyombo vya habari vyenye nguvu ya uhuru, ni sawa na kuwa na miundombinu bila waandishi wa habari,” amesema Ulimwengu na kuongeza kuwa uhuru wa vyombo vya habari na waandishi wa habari utakuwa na tija kwa umma.
Mhariri Mwandamizi na Mshauri wa Vyombo vya Habari nchini, Jesse Kwayu amesema wamiliki wana nafasi kubwa ya kusaidia vyombo vya habari kufanya kazi kwa uhuru, uwazi na haki, badala ya kuingilia na kudidimiza dhana hizo.

“Uwazi una thamani kubwa kwa umma, ni ishara ya utawala bora, unawezesha jamii kuwa huru kila kitu,” Kwayu amesema.

Afisa Habari na Msimamizi wa Mradi wa MISA Tanzania Jacqueline Jones amesema majadiliano hayo yanalenga kuimarisha uhuru wa habari nchini na kwamba taasisi hiyo inashirikiana na International Media Support (IMS) katika juhudi hizo, kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).
Mweka Hazina wa MISA Tanzania, Michael Gwimile akifungua Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri kwa niaba na Mwenyekiti wa MISA Tanzania Salome Kitomari leo Jumatano Desemba 15,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
 Mweka Hazina wa MISA Tanzania, Michael Gwimile akifungua Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri kwa niaba na Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Salome Kitomari.
Kaimu Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Andrew Marawiti akizungumza wakati wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.
Kaimu Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Andrew Marawiti akizungumza wakati wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.
Afisa Habari na Msimamizi wa Miradi MISA Tanzania,  Jacqueline Jones akizungumza wakati wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.
Afisa Habari na Msimamizi wa Miradi MISA Tanzania,  Jacqueline Jones akizungumza wakati wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.
Mwandishi wa Habari Mwandamizi nchini Tanzania Jenerali Ulimwengu akizungumza wakati wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.
Mwandishi wa Habari Mwandamizi nchini Tanzania Jenerali Ulimwengu akizungumza wakati wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.
Mwandishi wa Habari Mwandamizi nchini Tanzania Jenerali Ulimwengu akizungumza wakati wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.
Mhariri Mwandamizi na Mshauri wa Vyombo vya Habari nchini Jesse Kwayu akizungumza wakati wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri.

Washiriki wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri wakiwa ukumbini

Washiriki wa Mjadala kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na Uhuru wa Kiuhariri wakiwa ukumbini.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments