WILAYA YA MISENYI YAKAMILISHA MIRADI YA UVIKO 19 KABLA YA MUDA ULIPANGWA



HALMASHAURI ya Wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera imefanikisha usimimizi wa fedha za miradi ya maendeleo ya  Uviko 19 iliyo tolewa na serikali kuu ,ambapo imeweza kutekeleza asilimia 95 ya miradi  53 ya vyumba vya madarasa ya sekondari kabla ya muda uliowekwa  ifikapo Desemba 15 Mwaka huu.

Hayo yamedhibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ya Misenyi ,Waziri Kombo mara baada ya  ziara yake na wataalamu wa Halmshauri hiyo kukagua miradi ambayo inatekelezwa.

Kombo amesema kuwa Halmashauri yake ilipewa Bilioni moja na milioni 60 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo ikiwemo ujenzi wa madarasa 53 ya wanafunzi wa kidato cha kwanza watakaoanza kidato cha kwanza mwakani na madarasa 10 ya shule shikizi za msingi.

Amesema mafanikio hayo ni kutokana na ufatiliaji wa karibu na wa mara kwa mara ulioenda sambamba na ushirikiano kati ya viongozi wote kuanzia walimu ambao walipewa jukumu la kusimamia mafundi,viongozi wa Wilaya,Chama mpaka Mkoa jambo ambalo limeleta tija kubwa.

Amesema kuwa uwepo wa madarasa hayo umewapunguzia mzigo wakurugenzi kwani ni jambo ambalo lilikuwa linawatesa kwamba watayajengaje ila kupitia fedha za Serikali itasaidia kuondoa changamoto hiyo na kuwasaidia wanafunzi kusoma bila shida.

‘’Tunamshukuru Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha kwa ajili ya miradi hii kwenye Halmashauri yetu,tulikuwa hatulali tulifatilia kwa karibu na kuna wakati tulitumia ukali kwa wasimamizi lakini lengo lilikuwa ni kutimiza maagizo tuliyopewa na hatimaye leo tumemaliza kabla ya wakati na kwa viwango vya juu’’amesema Kombo

Kwa upande wao wataalamu ngazi ya  Halmashauri hiyo katibu kamati ya ufatiliaji miradi ya uviko 19 ,Gozberth  Bernard na mhandisi Lucy Nshoma wamesema kuwa mradi huo ulikuwa na usimamizi mzuri na wenye viwango bora vilivyotolewa na serikali.

Wakizungumza kwa nyakati fofauti wananchi wa Wilaya ya Misenyi wamesema kuwa wanaishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa jinsi ilivyoleta maendeleo kwenye jamii hususani madarasa ambayo yatasaidia Watoto wao kupata elimu bora.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments