MWANAMKE MWENYE VIRUSI VYA UKIMWI APONA BILA KUTUMIA DAWA

Mwanamke kutoka nchini Argentina anaonekana kupona kutokana na virusi vya ukimwi bila ya kutumia madawa au kupata matibabu - kikiwa ndicho kisa cha pili cha aina hiyo kuwahi kutokea duniani.

Madaktari wanaamini kuwa mfumo wa kinga ya mwili wa mgonjwa huyo ulisafisha kirusi hicho.

Vipimo kwa zaidi ya seli zake bilioni moja viligundua kuwa hakukuwa na dalili zozote za maambukizi.

Iwapo mfumo huu utatumiwa unaweza kugundua njia ya kumaliza au kutibu virusi vya HIV, kulingana na wataalamu.

Kumaliza HIV

Matokeo hayo ni thibitisho zaidi kuwa watu wachache wanazaliwa wakiwa na kinga dhidi ya HIV. Wengine wana jeni zinazozuia maambukizi.

Wengine - akiwemo mgonjwa wa Esperanza ambaye hataki kutajwa jina - wanaonekana kuambukizwa lakini baadaye wanatokomeza kirusi hicho.

Lakini watu wengi walio na HIV wanahitaji dawa za kupunguza makali ya kirusi hicho ya (ART).

Na iwapo wataacha kutumia dawa hizi, kirusi hicho kinaweza kuamka tena na kusababisha matatizo tena.

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ripoti za wale wanaojulikana kama "elite controllers" wanaoweza kuondoa kirusi hicho bila ya msaada wa dawa.

Adam Castillejo, kutoka London aliacha kunywa dawa za kila siku za HIV baada ya kupata matibabu ya saratani, ugonjwa ambao pia alikuwa nao.

Seli zilizokuwa na HIV zilitokomezwa wakati akipata matibabu ya saratani.

'Tiba ya kinga ya mwili'
Lakini mgonjwa wa Esperanza hakuwa na HIV iliyotambuliwa kwa zaidi ya miaka nane.

Loreen Willenberg, kutoka San Francisco pia anaoneka kupona kutokana na virusi vya HIV kwa njia ya kinga yake ya mwili

Ni hii inatoa matumaini kwa wagonjwa amboa miili yao inaweza kutibu HIV.

Mtafiti mkuu Dr Xu Yu kutoka taasisi ya Ragon ya hospitali ya Massachusetts anasema huenda kuna njia ya kuweza kuwatibu watu ambao hawana uwezo wa kufanya hivyo wenyewe.

'Maambukizi yaliyofeli'

Prof John Frater, kutoka chuo cha Oxford aliiambia BBC kuwa ni vigumu kuamua ikiwa mtu amepona kabisa kutokana na HIV.

Swali kuu ni iwapo mgonjwa amefanikiwa kupona mwenyewe au kwa njia nyingine.

"Kinga yake ya mwili inaonyesha wazi kuwa alikuwa na kirusi hicho, kwa hivyo hakuna swali iwapo alikuwa hivyo.

Huenda kuna wagonjwa kama hao pale nje, wanaoweza kusaidia kwenye utafiti kuhusu tiba ya HIV.

Prof Sarah Filder mtaalamu wa HIV katika chuo cha Imperial mjini London anasema kazi hiyo itasaidia kuboresha tiba za kinga ya mwili ambazo kwa sasa zinafanyiwa utafiti.

Lakini Dr Andrew Freedman, kutoka chuo cha Cardiff Medical School anasema madawa ya sasa ya kutibu HIV ni mazuri na licha kuwa kutafuta matibabu zaidi ni muhimu, kuhakikisha madawa ya ART yanafika kote duniani ndilo suala muhimu kwa sasa.

Chanzo - BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments