NGONO YA 3000 YAELEZWA KUUMIZA WAVUVI - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, November 23, 2021

NGONO YA 3000 YAELEZWA KUUMIZA WAVUVIMHITIMU wa Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo cha Afya KCMC katika taaluma ya Huduma ya Afya ya Jamii, Maseke Mgalo ameeleza kuwa tafiti aliyofanya juu ya upatikanaji na utoaji wa huduma ya afya ya jamii, amebaini kuwa kundi la wavuvi linaendelea kupata maambukizi ya VVU kutokana na mazingira yao.

“Licha ya mtu wa kwanza Afrika kupata maambukizi ya VVU alitoka katika kundi la wavuvi bado kundi hilo halifikiwi kwa urahisi kupatiwa elimu ya afya kutokana na mazingira yao pamoja na tabia yao ya kununua ngono.

“Nilifanya utafiti wangu Mkoa wa Mwanza na Mara vijijini wavuvi bado wana hatari ya kupata mambukizi ya VVU kwani bado wanafanya biashara ya ngono hadi Tsh 3000, hii ni hatari nimependekeza serikali ipeleke elimu huko kunusuru kundi hilo muhimu kwa jamii,” Maseke Mgalo, Phd.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages