Breaking

Post Top Ad

Thursday, November 11, 2021

TAPELI WA MAPENZI AKAMATWA KWA KUWADANGANYA WANAWAKE ATAWAOA...ANAHONDOMOLA TU


Polisi kutoka Nallagonda, India siku ya Jumanne, Novemba 9,2021 wamemkamata mwanaume mmoja ambaye amekuwa akiwalaghai wanawake akiahidi kuwa atawaoa.

Mwanaume huyo mmoja alikuwa akiwalaghai wanawake akiahidi kuwa atawaoa.

 Mtuhumiwa huyo anaripotiwa kwamba hupiga kinanda na kuimba kanisani.

 Wakati wa kukamatwa kwake, mwanamume huyo alizua sarakasi akijifanya kuwa na mshtuko wa moyo.

Ulaghai wa mapenzi Mtuhumiwa huyo.

Tulakoppula Samuel Williams anaripotiwa kwamba hupiga kinanda na kuimba kanisani katika Kituo cha Clock Tower, Nallagonda.

 Williams alitambulishwa kwa mwanamke kutoka Srinivasnagar katika mji huo ambaye alikuwa ametengana na mumewe sababu ya ugomvi wa kifamilia. 

Mwanamke huyo ambaye alikuwa mjamzito, alinyanyaswa kingono na Williams na kisha walianza kuishi pamoja kwa miaka 9.

Williams ambaye pia alianzisha shirika la hisani la YMCA, alikuwa ameahidi kumupa mrembo huyo atampa kazi katika shirika hilo baadaye.

Lakini badala yake alimpa mwanamke mwingine kazi katika shirika hilo na kuishi naye kwa miezi sita kabla ya kumuoa Oktoba 25, 2021.

 Njia ya mwongo ni fupi

 Wakati mwanamke kutoka Srinivasnagar alipogundua Williams ameoa mwanamke mwingine, ugomvi ulizuka kati ya wawili hao na kujaribu kumshambulia kwa kisu. 

Alikimbia kupiga ripoti kwa polisi lakini maafisa walipojaribu kumkamata mtuhumiwa, aliruka ukuta kutoka nyuma na kukimbia.

 Ulaghai wa Williams ulitambulika maafisa wa polisi walipokuwa wakifanya uchunguzi wa na kutambua kuwa alikuwa katika uhusiano na wanawake wengine kadhaa nje ya nchi.

 Alipa fidia ya mamilioni kwa kumtema ex wake

Katika sarakasi nyingine ya mapenzi, mrembo Mnigeria alimshtaki mpenzi wake wa zamani ambaye alimtema na kuoa mwanamke mwingine. 

Mrembo huyo alikuwa ameposwa na mpenzi wake wa zamani na walikuwa wanatazamiwa kufanya harusi. 

Hata hivyo, jamaa huyo alivunja ahadi ya kumuoa mrembo na badala yake kumtema na kufanya harusi na mwanamke mwingine.

Akiwa amevunjika moyo na machungu ya kuwaachwa, mrembo huyo alimburuta mpenzi wake wa zamani kortini na kutaka alipwe kima cha KSh1.5 milioni na gari kama fidia.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages