Breaking

Post Top Ad

Thursday, November 11, 2021

MWANAFUNZI ALIWA NA MAMBA AKIOGA ZIWA VICTORIA
Mwanafunzi wa darasa la nne Shule ya Msingi Nyakasasa, aitwaye Ntogoso Gunya (12) amefariki dunia baada ya kuliwa na mamba wakati akioga kando ya Ziwa Victoria mkoani Mwanza.

Tukio hilo limetokea jana Jumatano, Novemba 10, 2021 saa 11 jioni na kuthibitishwa na mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga.

Juhudi za kuutafuta mwili wa merehemu zilianza jana ambapo leo asubuhi wamefanikiwa kupata kichwa pekee huku kiwiliwili na sehemu zingine za mwili wa mwanafunzi huyo zikiwa zimeliwa.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages