JWTZ YATOA UFAFANUZI KUHUSU MATAPELI WA AJIRA JESHINI - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, November 30, 2021

JWTZ YATOA UFAFANUZI KUHUSU MATAPELI WA AJIRA JESHINIJeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limetoa ufafanuzi kuhusu vitendo vya rushwa, ulaghai na utapeli vinavyofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu, wakiwaahidi watu mbalimbali kwamba watawasaidia kupata nafasi ya kuandikishwa katika nafasi za ajira zilizotangazwa na jeshi hilo.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 30, 2021 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jeshi, Upanga jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Habari Jeshini, Gaudentius Ironda, amesema matapeli hao wameenda mbali zaidi na kutumia jina la mkuu wa majeshi, wakieleza kwamba ndiye aliyewatuma kukusanya fedha ili wapate nafasi ya kuandikishwa, jambo ambalo si la kweli.


Amewataka wananchi kutoa taarifa haraka endapo watakutana na watu wa aina hiyo, na kusisitiza kwamba jeshi halina utaratibu wa kuwatoza watu fedha ili wapate nafasi ya kujiandikisha na kwamba wanaofanya vitendo hivyo ni matapeli.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages