Breaking

Post Top Ad

Saturday, November 13, 2021

VIJANA WASHINDWA KUOA KWA SABABU YA MAKAHABA ...DIWANI AOMBA KONDOMU

JESHI la Polisi wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani limesema vijana wanashindwa kuoa mapema kwa sababu huduma ambayo walipaswa kupatiwa na wake zao baada ya kuoa wamekuwa wakiipata kwa bei nafuu kutoka kwa wadada poa wanaofanya biashara ya ngono wilayani humo.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wilaya ya Kisarawe, Eva Steshen wakati wa ziara iliyofanywa na kamati ya UKIMWI iliyobaini kuwepo kwa madanguro wilayani humo.

Aidha, madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo wamesema kufuatia kuibuka kwa vikundi vya wasichana wanaojihusisha na uuzaji wa miili yao wilayani humo, wameanzisha mpango wa kuwapatia elimu ya ujasiriamali na mikopo kama mitaji itakayowawezesha kuachana na vitendo hivyo badala ya kuwafukuza.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata wa Kibuta wilayani Kisarawe mkoani Pwani Mhandisi Mohamed Kilumbi, amesema kuwa Kata ya Mbuyuni wilayani humo inakabiriwa na upungufu mkubwa wa Condom na kuiomba kamati ya kupambana na UKIMWI kuchukulia kwa uzito jambo hilo na kuharakisha kuzipeleka.
 
Chanzo - Global publishers

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages