Breaking

Post Top Ad

Saturday, November 13, 2021

MWANZILISHI WA WEAKLEAKS ARUHUSIWA KUFUNGA NDOA GEREZANI


Mwanzilishi wa mtandao maarufu wa Wikileaks, Julian Assange ameruhusiwa kumuoa mpenzi wake Stella Moris katika gereza la Belmarsh nchini Uingereza. Assange na Bi Moris wana watoto wawili wa kiume, ambao waliwapata wakati wakiishi katika ubalozi wa Ecuador mjini London.

Huduma ya jela hiyo imesema kwamba ombi la Assange liliruhusiwa na gavana wa jela hiyo. Bi Moris alisema kwamba amefurahi kwamba ombi lao limepokelewa. Aliongezea kwamba: “Nadhani hakutakuwa tena na usumbufu mwengine wa ndoa yetu.”

Wafungwa wana haki ya kuomba kufunga ndoa wakiwa jela chini ya kifungu cha ndoa cha 1983 na ombi hilo linaporuhusiwa wanapaswa kusimamia gharama zote za ndoa hiyo bila usaidizi wowote wa fedha za umma.

Katika mahojiano na gazeti la Mail la siku ya Jumapili mwaka uliopita, Moris, wakili wa Afrika Kusini, alifichua kwamba alikuwa katika uhusiano na Assange tangu 2015 na amekuwa akiwalea watoto wao wawili yeye binafsi.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages